27 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mbalizi na Uyole wapewa elimu ya Kodi kuhusu utunzaji kumbukumbu

RACHEL MKUNDAI – MBEYA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kutoa elimu ya Kodi kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mbeya katika kampeni maalumu ya Elimu ya Kodi mkoa kwa mkoa.

Kampeni hiyo iliyoanza tangu Machi 9, inaendelea hadi Machi 14 ambapo wafanyabiashara wa eneo la Mbalizi na Uyole wamepewa elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara ili waweze kulipa Kodi sahihi na kwa wakati.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Huduma na Elimu kwa mlipakodi wa mkoa wa Mbeya, Serapio Luanda amesema TRA inalenga kutoa elimu ya Kodi kwa wafanyabiashara na wananchi wa mkoa wa Mbeya ili kila mfanyabiashara atambue haki na wajibu wake katika kulipa kodi ikiwa ni pamoja na wajibu wa TRA kama mkusanyaji Kodi za serikali.

Aidha amewataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara kwani ndicho kigezo kikubwa kinachotumika wakati wa ukokotoaji wa Kodi ambayo mfanyabiashara anastahili kulipa kwa mujibu wa sheria za Kodi.

“Tunafanya kampeni ya Elimu ya Kodi kwa wafanyabiashara na wananchi ili wafahamu sheria za Kodi na utaratibu unaotumiwa na TRA katika ukusanyaji wa Kodi” amesema Luanda.

Amesema TRA inafanya kampeni ya elimu ya Kodi mkoa kwa mkoa ikilenga kuwaelimisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla masuala mbalimbali yanayohusu ulipaji kodi ikiwemo haki na wajibu wa Mlipakodi, umuhimu wa utunzaji wa kumbukumbu za biashara, madhara ya biashara za magendo mipakani pamoja na njia za kielektroniki za ulipaji kodi ya majengo na Kodi za mapato kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles