29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mauaji yakatiza ziara ya Rais wa Mali

BAMAKO-MALI

SIKU moja baada ya kuripotiwa mashambulizi mabaya yaliyosababisha mauaji ya watu 100 katika kijiji cha Dogon kilicho eneo la kati nchini Mali,  Rais wa nchi hiyo, Ibrahim Boubacar Keita amesema anakatiza ziara yake nchini Uswisi kutokana na mauaji hayo.

 Rais huyo amelaani vikali mauaji hayo jana wakati  akizungumza na raia wa Mali wanaoishi nchini Uswisi.

Maofisa wa nchi hiyo  wamesema hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mashambulizi hayo yaliyosababisha pia watu 19 kutoweka.

Hata hivyo Moafisa wa Serikali za Mitaa,  wamedai kuwa kundi la wapiganaji linaloaminika kuwa ni wa jamii ya kabila la Fulani walivamia kijiji cha Dogon katikati mwa Mali usiku wa Jumapili, na kuwaua watu wapatao 95 na kuzichoma moto nyumba kadhaa.

Mauaji hayo yaliyowalenga jamii ya wadogon, yanaibua makovu ya mashambulizi ya kikabila ambayo tayari yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha.

Mauaji hayo yametokea chini ya kipindi cha miezi mitatu baada ya karibu raia 160 wa kabila la Fulani walipouawa na kundi linalojulikana kama Dogon.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Eri Kaneko amewaambia waandishi wa habari mjini New York kwamba wanajeshi wa kulinda amani wa kikosi cha anga wa Umoja wa Mataifa walitoa msaada kwa serikali ya Mali katika jitihada za kuzuia mashambulizi zaidi.

Vurugu kati ya jamii ya Dogon ambao ni wawindaji na wafugaji wa kabila la Fulani zimesababisha vifo vya  mamia ya watu tangu mwezi Januari.

Katika shambulio la mwezi Machi wafugaji zaidi ya 150 wa kabila la Fulani waliuawa ikiwa ni mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi ya umwagaji damu kuwahi kutokea katika historia ya hivi karibuni ya Mali.

Itakumbukwa mwaka 2013 majeshi ya Ufaransa yaliingilia kati nchini Mali iliyokuwa zamani koloni lake ili kupambana na makundi ya jihadi kutoka eneo la kaskazini lakini makundi hayo ya wanamgambo wa zamani yamejikusanya tena upya.

AFP/APE

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles