26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yataifisha mali zenye thamani ya Sh bilioni 93.16

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Serikali imetaifisha mali za wahalifu zenye thamani ya Sh bilioni 93.16 kuanzia mwaka 2013 hadi Mei, mwaka huu zilizokamatwa kwenye sekta za Madini, Maliasili na Sekta ya fedha (Upatu) ikiwa ni sehemu ya kudhibiti uhalifu kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Uhalifu huo unaodaiwa kukithiri katika miaka ya nyuma na ambao sasa unaendelea kudhibitwa unatajwa kuliingizia Taifa hasara ya mabilioni  ya fedha, hatua iliyoifanya Serikali kuudhibiti kwa kutaifisha mali za wahusika wa uhalifu huo.

Hayo yamesemwa leo Juni 12, jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, wakati akifungua mkutano wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Taasis za Urejeshaji wa mali zinazotokana na uhalifu Kusini mwa Afrika (ARINSA) wenye jumla ya nchi  wanachama 16.

Samia amesema hivi sasa Serikali ya Tanzania inapanga mikakati ya kuondokana kabisa na uhalifu huo kutokana na sera ya kudhibiti rushwa pamoja na kuanzisha mahakama maalum zitakazoshughulikia ufisadi hapa nchini.

“Sisi Tanzania tunaimarisha sera zetu za kupambana na Rushwa na Ufisadi, tunaenda sambamba na umoja wetu huu wa ARINSA hivyo tunazishauri nchi zingine ambazo zipo kwenye umoja huu na bado hazijatunga sera na sheria ziharakishe mchakato ili twende sawa,” amesema Samia.

Kwa upande wake Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Augustine Mahiga amesema mkutano huo pamoja na mambo mengine utazungumzia mikakati ya pamoja ya kudhibiti uhalifu wa mipakani hasa kwenye udhibiti wa uingizwaji wa bidhaa haramu zikiwamo dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Maganga, amesema mkakati wa kutaifisha mali za wahalifu umekuja kufuatia kuona vifungo gerezani kwa wahalifu hao havitazinufaisha nchi hizo na badala yake kuchukua mali zao ili kukomesha kabisa suala hilo.

Aidha amesema tayari wataalamu kadhaa wa upelelezi wa kufuatilia mali na kuzitaifisha wameshapata mafunzo na kwamba zoezi hilo linaendelea ili kuhakikisha linafanyika kikamilifu na kwa usiri mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles