BEIJING, CHINA
WAJUMBE wa China na Marekani wanaendelea na mazungumzo ya biashara siku ya tatu jana kwa lengo la kumaliza vita vya ushuru baina ya nchi hizo mbili.
Hilo linakuja huku Rais wa Marekani, Donald Trump kupitia mtandao wa Twiter akitupia ujumbe usemao mazungumzo kujadili vita vya ushuru baina ya nchi hizo mbili yanaendelea vizuri sana.
Hatua ya kuendeleza majadiliano ya bishara ambayo awali yalikuwa yafanyike kwa siku mbili tu, imesababisha kuongezeka kwa biashara kwenye masoko ya hisa ya Asia.
Wajumbe wa China na Marekani wanakutana kwa mara ya kwanza tangu Trump na mwenzake wa China, Xi Jinping kukubaliana Desemba mwaka jana kuwa wataepusha hatua zaidi za adhabu katika uagizaji kati ya nchi zao kwa muda wa siku 90 wakati majadiliano yanapofanyika.