27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mapigano wakulima, wafugaji yaibuka Monduli

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro Akishirikiana wananchi kumwingiza kwenye gari mmoja wa majeruhi wa mapigano ya wafugaji yaliyosababisha maboma zaidi ya 20 kuchomwa moto katika Kijiji cha  Mfereji mpakani mwa Wilaya ya Monduli na Arumeru mkoani Arusha jana.

ELIYA MBONEA, ARUSHA

TAKRIBANI watu 400 kutoka wilayani Arumeru, wanadaiwa kukivamia Kijiji cha Mfereji kilichopo Monduli mpakani na kutembeza kipigo usiku wa nane na kuharibu mali na mifugo.

 Chanzo cha mapigano hayo inadaiwa ni mgogoro wa muda mrefu wa mpaka kwa wananchi hao unaohusisha eneo la malisho ya mifugo ya wananchi wa jamii ya Kimaasai wanaoishi mpakani mwa wilaya hizo mbili.

Vurugu hizo zimeelezwa kusababisha hasara kwa wananchi wa Kijiji cha Mfereji kilichopo Monduli kutokana na maboma yao zaidi ya 20, mifugo, vyakula na nyumba kuchomwa moto hatua iliyiosababisha zaidi ya kaya 100 kukosa mahali pa kuishi.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo lilitokea kuanzia saa  3 hadi Saa 7 usiku, walisema watu hao walikuwa na silaha za jadi.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu Mbunge wa Jimbo la Monduli (CCM), Julius Kalanga, alisema hakuna kifo kilichotokea japo baadhi ya wananchi walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Monduli kwa matibabu.

 “Kuna mwana nchi mmoja alilazimika kukimbizwa hospitali kwa matibabu hali yake haikuwa nzuri sana na kwa sasa nimeambiwa anahamishiwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru,” alisema Kalanga na kuongeza:

 “Nimekuwa hapa kuwatuliza wananchi wangu wasilipize kisasi kwani Serikali itahakikisha inashughulikia suala hili, kwa ujumla wananchi hawana mahali pa kuishi nyumba zao zimechomwa moto pamoja na vyakula,”alisema.

Kalanga alisema mgogoro huo ni wa muda mrefu ambapo unahusisha mpaka kati ya wananchi wanaoishi upande wa Mfereji wilayani Monduli na Arumeru.

 “Septemba mwaka jana Waziri wa Ardhi William Lukuvu alitembelea Monduli aliagiza mgogoro huo ushughulikiwe ikiwa ni pamoja na kuanisha maeneo ya mipaka.

“Jambo la kusikitisha maagizo hayao hayakufanyiwa kazi mpaka kumetokea vurugu hizi zilizosababisha uharibifu wa mali na mifugo,” alisema Kalanga.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Murro,  akizungumza eneo kulipotokea vurugu hizo alisema, Serikali ya wilaya itahakikisha inachukua hatua kwa wote waliohusika na vurugu hizo.

 “Kwa watakaobaika kufanya vurugu hizi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao bila kujali wana nyadhifa zipi, hatuwezi kukubali kuona wananchi wakiishi kwa wasiwasi kwenye nchi yao hili halitakubalika.

 “Na hatua hizi zitakomesha mgogoro huu  unaotajwa kudumu kwa zaidi ya miaka 40,” alisema.

Naye Mkuu wa wilaya ya Monduli, Idd Kimanta, aliyekuwa kwenye eneo la tukio, alisema watu takribani 400 hawawezi kuvamia kijiji bila ungozi kufahamu.

 “Niwaombe wananchi wa Monduli msilipe kisasi, Serikali tayari inaanza uchunguzi wa kina ili kuwabaini wahusika hapa lazima baadhi ya viongozi wanahusika tulieni Serikali inafanya kazi yake,” alisema Kimanta.

mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles