28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Lipumba, Maalim Seif kicheko au kilio leo

MWANDISHI WETU    

NI kicheko ama kilio. Ndivyo unaweza kusema leo hasa baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, itakavyoamua hatima ya uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba dhidi ya kesi iliyofunguliwa na upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.

Kesi hiyo inatarajiwa kutolewa uamuzi na Mahakama Kuu chini ya Jaji Dk. Benhajj Masoud, ambapo itaamua hatima ya mgogoro ndani ya chama hicho uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Benhajj Masoud, kutengua bodi ya upande wa Lipumba pamoja na kusema kuwa hata ile ya upande wa Katibu Mkuu Maalim Seif nayo haina uhalali kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

Kutokana na hali hiyo juzi Maalim Seif aliitisha kikoa cha Baraza Kuu na kuhudhuriwa na wajumbe 37, ambapo walipiga kura na kuchagua wajumbe wanane wa bodi ya wadhamini huku akisema kuwa Lipumba hana watu ndani ya chama na hana wajumbe wa baraza wanamuonga mkono.

Jana naye Profesa Lipumba ambaye anatambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, alijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kutangaza wajumbe wajumbe wa bodi wa wadhamini ya chama hicho.

Hatua hiyo ilikuja siku mbili baada ya CUF upande wa Maalim Seif Sharif Hamad nao kuteua wajumbe hao.

Katika mkutano huo, Profesa Lipumba aliwatangaza wajumbe hao walioteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho kuwa ni  Peter Malebo, Abdul Magomba, Hajra Silia, Amina Mshamu nq Aziza Daghesh , Salh Hilal Mohammed, Asha Said Suleiman, Suleiman Makame Issa na Mussa Haji Kombo.

“Wajumbe hawa wameteuliwa baada ya Baraza Kuu la Uongozi wa CUF kukutana Februari 19, 2019. Kikao hiki kilihudhuriwa na Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza kama taratibu zinavyotaka,” alisema ProfesaLipumba

Profesa Lipumba, alisema baada ya kuteua wajumbe hao wameshawalisha barua ya maombi ya kuisajili bodi katika Ofisi ya Wakala Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA)  pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Mwenyekiti huyo wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, alisema wajumbe wa  bodi ya wadhamini walioteuliwa na upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif hawatambuliki kwa kuwa upande huo hauna Baraza Kuu la Uongozi wala Kamati ya Utendaji.

“Ama kweli lakini kilichonisikitisha ni namna alivyowateua wajumbe hawa, yaani Maalim Seif katika huo mkutano wa uteuzi wa wajumbe alimualika Jacob (Boniface – Meya wa Manispaa ya Ubungo) na Mbatia (James-Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) kushuhudia tukio hilo. Hivi hawa wanawajua vizuri wajumbe wa Baraza Kuu la CUF?

“Huyu (Maalim Seif) si mtu mzuri anataka kukiua chama hiki na hana nia ya dhati dhidi ya CUF. Nawaambia bodi halali ni iliyotangazwa leo (jana) na si vinginevyo na nina imani RITA itatenda haki katika hili,” alisema Profesa Lipumba

Hata hivyo kauli za viongozi hao wawili kati ya Profesa Lipumba na Maalim Seif Sharif Hamad, zinaonesha wazi kuwa mgogoro wa wawili hao bado ni mbichi, pamoja na kuwapo kwa jitihada kadhaa za kuondoa tofauti zao.

Profesa Lipumba alitangaza kujiuzulu uenyekiti, Agosti 5, 2015 lakini baada ya mwaka mmoja akatengua uamuzi huo na kutangaza kurejea katika wadhifa huo jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles