29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Majukwaa ya wanaume yapigiwa chapuo tamasha la jinsia

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Phumzile Ngcuka amesema kuna haja ya kuwa na majukwaa ya wanaume kwa lengo la kupinga ukatili wa kijinsia.

Akizungumza leo Novemba 7,2023 wakati wa Tamasha la Jinsia la 15 lililokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), amesema wanaharakati wa kifeminia wanapaswa kujikita kuelimisha kuhusu ulinzi wa mtoto wa kiume kwa mustakabali wa haki na usawa wa kijinsia.

Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP.

Amesema moja ya mambo ambayo yamekuwa yakiendeleza ubaguzi ni mfumo dume na kutaka wanaume kuupinga kwani karne ya sasa inahitaji wanaume wenye mshikamano.

“Mfumo dume haufai kwa wanawake na wanaume lakini unaendeleza ubaguzi, hivyo wanaume na watoto wa kiume hawana budi kuwa sehemu muhimu ya harakati hizi.

“Hatutaweza kupiga hatua kama hatutatokomeza mfumo dume, wanaume waseme namna watakavyopambana na mfumo dume na kuutokomeza,” amesema Ngucuka.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gema Akilimali, amesema bado kuna changamoto nyingi hivyo mshikamano na serikali unahitajika kwa sasa kuliko huko walikotoka.

Alisema tamasha hilo la siku nne litatoka na maazimio ya jumla kwani upo mchango wa TGNP katika harakati mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi, alisema tamasha hilo linawakutanisha pamoja watu wa ukanda wa Afrika ambapo wameendelea kusimama kwenye misingi ya waasisi wao.

“Tamasha la jinsia ni jukwaa la kuleta sauti kwa paamoja, kujadili na kupanga mikakati. Hili ni tamasha la 15 tangu kuanzishwa na limeshirikisha washiriki zaidi ya 2,000,” alisema Liundi.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalumu, Timoth Mgonja, amesema maazimio yote yatakayotokana na tamasha hilo yatakuwa ni kitendea kazi kwao kwa kuwapa ramani pana ya kushughulikia changamoto mbalimbali zilizoko katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles