30.8 C
Dar es Salaam
Monday, June 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mahitaji ya Virutubishi vya chakula ni ajenda yua Kitaifa-Mhagama

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema mahitaji ya virutubishi vya chakula ni ajenda kubwa ambayo itachochea katika kuongeza ajira kwa wakulima na kuwa na uhakika na virutubishi vinavyotumika hapa nchini.

Nyangwaka Ndili kutoka Jukwaa la Wasindikaji akieleza jambo mbele ya Waziri wa Nchi alipotembelea na kufanya kikao na watendaji wa Kiwanda cha Sanku kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Waziri Mhagama ameyasema hayo alipotemebelea na kukagua kiwanda cha Sanku kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam Mei 25,2024 na kujionea maendeleo ya kiwanda hicho cha uchanganyaji wa virutubishi kwenye unga wa mahindi na ngano kwa bei nafuu.

Aidha, amehimiza kiwanda hicho kuendelea kufanya ufuatliaji wa karibu katika kutoa elimu ili kuondoa matatizo mengine ya udumavu, utapiamlo na shida ya kupungukiwa vitamini A kwa wakinamama wajawazito.

“Hii kazi ni yenye manufaa makubwa na itaweza kutusaidia sana kama nchi tuweze kusonga mbele na kusaidia kuitangaza nchi kwa kuwa na kiwanda kikubwa cha kuchanganya virutubishi,” alisema Waziri Mhagama.

Mhandisi Joseph Mtwangi akieleza jambo mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Jensita Mhgama juu utendaji kazi wa vifaa mbalimbali katika kiwanda cha Sanku.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Sanku, Gwao Omari Gwao, amesema kampuni yao inasaidia wafanyabishara wadogo na wakati kufanya urutubishaji ambazo zimefunguliwa katika Mikoa 26 Tanzania Bara na katika Halmashauri 142 Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles