31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Liverpool yakaribisha wasafiri kutoka ndani, nje

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Uwekezaji wa Sh milioni 500 uliofanywa katika mgahawa wa Liverpool umekuwa kivutio kwa abiria wanaosafiri ndani na nchi jirani.

Mgahawa huo uliopo katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ulioanzishwa mwaka 1993 umefanyiwa maboresho makubwa ambapo pia kuna sehemu ya kukaa watu mashuhuri (VIP).

Akizungumza Februari 18,2024 na waandishi wa habari Meneja wa Mgahawa wa Liverpool, Salim Abdallah, amesema wamekuwa wakihudumia wasafiri mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

“Tunatoa huduma ya chakula kwa saa 24, tunawahakikishia wasafiri wote wa mikoani na nchi jirani kwamba huduma zetu ni nzuri na zenye ubora unaotakiwa.

“Bei zetu ni rafiki haziwaumizi Watanzania kwa sababu tunajua wako wengine ambao wana vipato vidogo,” amesema Abdallah.

Amesema kwa sasa wafanyakazi zaidi ya 30 wameajiriwa katika mgahawa huo na kuahidi kutoa huduma bora zaidi.
“Vyakula vyetu ni salama kwa sababu tunazingatia kanuni za afya, vyoo ni visafi wakati wote na vipo vya kutosha hata mabasi matano yakiingia kwa wakati mmoja tunaweza kuyahudumia…tumeweka lami ili wakati wa mvua wasafiri wasipate adha ya kukanyaga tope,” amesema.
Katika hoteli hiyo pia kunauzwa matunda mbalimbali yakiwamo machungwa na matunda damu ambayo yanapatikana kwa wingi mkoani Tanga.

Mmoja wa abiria aliyekuwa akielekea mkoani Arusha, Rachel Mosha, amesema huduma za mgahawa huo ni nzuri na hajawahi kupata shida yoyote ya kiafya.

“Unaweza kula chakula sehemu nyingine ukaharisha lakini kwa Liverpool hii mara yangu ya nne sasa nakula hapa sijawahi kupata shida yoyote na bei zao ni nafuu,” amesema Rachel.

Uongozi wa Liverpool umemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini hatua iliyovutia wawekezaji katika sekta mbalimbali.

Rais Samia amekuwa akisema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kwani Tanzania ni salama na ina eneo bora la kuwekeza kutokana na kuwa na vivutio vingi vya utalii

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles