29.9 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Leo ni siku ya bajeti

Dk. Philip Mpango,Khamis Mkotya, Dodoma

MACHO na masikio ya Watanzania leo yataelekezwa mjini Dodoma,   Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, atakapowasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2016/2017.

Dk. Mpango anawasilisha bajeti hiyo sambamba na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambazo mawaziri wake wa fedha nao watawasilisha bajeti za nchi zao leo.

Bajeti hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Serikali ya Awamu ya Tano ni ya zaidi ya Sh trilioni 29,  asilimia 40 ikiwa imeelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Bajeti za wizara

Bajeti za wizara mbalimbali zilizowasilishwa bungeni tangu Bunge la Bajeti lilipoanza Aprili 19, zimekuwa zikionyesha   mwelekeo wa bajeti kujikita katika kutekeleza miradi na kuboresha huduma za wananchi.

 Katika kuhakikisha huduma za wananchi zinaboreshwa, Kamati ya Bunge ya Bajeti ilipendekeza bajeti ifumuliwe katika baadhi ya maeneo muhimu ambayo yametengewa fedha kiduchu.

Maoni ya wabunge

Baadhi ya wabunge waliozungumza na MTANZANIA jana walitoa maoni yao kuhusu bajeti itakayosomwa leo, huku wengine wakiwa na matumaini kuwa   itajibu kero na matatizo ya wananchi.

Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni (CCM), alisema  anatarajia bajeti hiyo itajibu matatizo ya wananchi   na kutekeleza ahadi zilitolewa na Rais Dk. John Magufuli wakati wa kampeni.

“Rais Magufuli aliahidi nchi ya viwanda yenye uchumi wa kati, Mpango wa Maendeleo uliotolewa leo (jana) una  miradi mikubwa, barabara, sekta za maji vyote naona vitaenda vizuri,” alisema.

Alisema changamoto iliyopo ni  kitendo cha Serikali kuzungumzia masuala ya viwanda bila kuwapo  maandalizi.

“Sekta ya viwanda haiwezi kuendeshwa na Serikali peke yake, ushiriki wa sekta binafsi unapaswa kuwa mkubwa kwa sababu tulishawahi zamani tuliona watu walichukua viwanda wakavitumia kinyume na ilivyopangwa,”alisema Dk. Chegeni.

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), alisema  hategemei makubwa katika bajeti hiyo kwa kuwa baadhi ya bajeti zilizowasilishwa zimetoa mwelekeo.

“Sitegemei mabadiliko makubwa katika bajeti kuu ingawa kuna baadhi ya wizara ambazo tunaona zitafanya mambo makubwa.

“Mfano Wizara ya Nishati na Madini tumeona fedha nyingi katika miradi ya umeme vijijini, Wizara ya Maji nayo tumeona imeelekeza fedha katika miradi ya maji vijijini nadhani huko ndipo tunaweza tukapiga hatua,”alisema Bobali.

Naye Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi (CCM) alisema  anategemea bajeti hiyo itaendana na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2016/17 na vipaumbele vyake ikiwamo ukuzaji wa uchumi wa viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles