23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Kwa Sh milioni 5 faru anapewa jina lako

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa za Tanzania (TANAPA) limeanzisha Programu maalum ya kuwezesha watu wanaotaka baadhi ya wanyama waitwe majina yao kufanya hivyo lakini kwa kulipia Sh milioni tano.

Hayo yameelezwa Jumatatu, Julai 24,2023 na Kamishna wa Uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2023/24.

Amesema wameanzisha programu ya kuwapa majina baadhi ya wanyama kwa kulipia Sh milioni tano.

“Hawa wanyama siyo wote labda kama umesema kuwa unampenda sana fisi unataka huyo fisi awe na jina lako,”amesema Mwakilema.

Amesema bodi ya menejimenti ya Tanapa imeshapitisha utaratibu huo ambao utaanza na wanyama aina ya faru.

Pia amesema mtu yeyote anaweza kumuona, kumuasili na atatakiwa kuchangia gharama za kumuhifadhi za Sh milioni 1 kila mwaka.

Amesema wapo baadhi ya faru pia wana majina akiwemo yeye mwenyewe ambaye mmoja wa faru katika Hifadhi ya Serengeti amepewa jina lake.

Hata hivyo, amesema
simba aliyepewa jina la Bob Juniour, alipewa na waongoza utalii baada ya kulinganisha mnyama huyo na msanii Bob Marley ambaye alivyokuwa na rasta.

Amesema isivyobahati jina hilo halikutambulika hadi alipokuja kufa akaanza kuvuma kuwa ndiye Bob Junior.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles