23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

KUPIMA MALARIA SASA NI BURE

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya na wafawidhi kuweka matangazo katika vituo vya afya, zahanati na hospitali  kuhusu huduma za upimaji wa malaria kwamba ni bure.

Agizo hilo alilitoa jana mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga wakati akizindua ugawaji wa vyandarua  vyenye dawa  ya muda mrefu kwa wajawazito  na watoto wenye umri wa mwaka mmoja.

Msaada huo umetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania  kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti malaria   na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID).

Ummy pia alipokea malalamiko ya wananchi wakidai kutozwa fedha kwa ajili ya matibabu wakati serikali imeagiza yawe bure.

Alisema ugawaji endelevu wa vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na Shirika la Johns Hopkins kupitia Mradi wa VectorWorks kwa ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kudhibiti malaria.

Waziri   alisema Ofisi ya Takwimu (NBS) mwaka  2017 zilionyesha kupungua kwa kiwango cha maambukizi ya malaria hadi chini ya asilimia 10  kutokana na mikakati iliyowekwa na wizara kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa huo.

“Niendelee kusisitiza dawa za malaria na matibabu ni bure, wananchi hawatakiwi kulipia, wafadhili wetu wanajitoa sana kuhakikisha malaria inaisha.

“Waganga wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na namba za simu kwenye vituo vya afya   wananchi watakaolipishwa  watoe malalamiko yao,” alisema Ummy.

Mwakilishi wa USAID Tanzania, Andy Karas alisema kwa miaka zaidi ya 12 wamefanya kazi ya kupambana na malaria kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na malaria ujulikanao kama PM

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles