33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kombora la Urusi gumzo

Moscow

WAHANDISI watano wa nguvu za kinyuklia waliofariki baada ya kulipuka injini ya roketi wamezikwa mjini Sarov, kilomita 373 mashariki mwa Moscow ambapo vichwa vya nyuklia hutengezwa.

Shirika la Serikali la usimamizi wa nguvu za kinyuklia nchini humo Rosatam lilisema wataalam hao walikuwa wakijaribu injini ya nyuklia.

Jaribio hilo lilifanywa karibu na ufukwe wa bahari ya Arctic. Urusi imekuwa ikijaribu kombora la kinyuklia kwa jina Burevesnik.

Mlipuko huo ulifuatiwa na kupanda kwa mionzi katika eneo la Seberodvinsk, mji uliopo yapata kilomita 40 mashariki mwa Nyonoksa karibu na bahari nyeupe.

Maafisa wa Severodvinsk wanasema mionzi hiyo ilifikia Microsierverts 2 kwa saa, kabla ya kurudi katika hali ya kawaida ya 0.11 Microsieverts.

Viwango vyote viwili ni vidogo mno kusababisha ugonjwa unaosababishwa na mionzi.

Wahandisi wengine watatu walijeruhiwa katika mlipuko huo na sasa wako hospitalini, Rosatom alisema.

Wataalam wa Urusi na magharibi wanasema kuwa jaribio hilo lilihusihswa na ndege wa baharini kwa jina Petrel.

Rais Vladimiri Putin alielezea kombora hilo katika hotuba yake bungeni mwezi Machi 2018.

Nato imelipatia umbo la SSC-X-9 Skyfall.

Mark Galeotti, mchanganuzi mkuu na mtafiti katika taasisi ya Rusi anasema kwamba urushaji wa kombora la kinyuklia unakabiliwa na changaomoto za kiufundi .

Kuna kasi dhidi ya uzito wa mfumo mbali na hatari ya kombora hilo kutoa mionzi kila mahali linapopitia , aliambia BBC.

Mfumo huo mpya ulianzishwa nyakati za Usoveiti – zilizotolewa zilikokuwa zikihifadhiwa na kuimarishwa . Injini ya Burevestnik inayoweza kurusha kombora la kinyuklia hauna uwezo wa kurusha kombora mbali kulingana na bwana Putin.

Lakini mlipuko wa Nyonoksa unaweza kuwa ulihusisha silaha nyengine ambayo pia ina uwezo wa kirusha kichwa cha nyuklia.

Ni nini kinachojulikana kuhusu mlipuko huo?

Wahandisi hao watano waliofariki walikuwa wataalam na mashujaa ambao walijua hatari zinazowakabili na walikuwa wamefanya majaribio mengine katika mazingira magumu zaidi alisema afisa mwanadamizi wa Rosatom Valentin Kostyukov .

Anaongoza kituo cha nyuklia cha Sarov – kituo kilichotumika wakati wa vita baridi kinachohusishwa na bomu lililotengezwa na hydrogen bomb nchini Urusi.

Aliwataja wahandisi hao kuwa Alexei Vyushin, Yevgeny Korotayev ,Vyacheslav Lipshev, Sergei Pichugin , Vladislav Yanovsky.

Awali wizara ya ulinzi ilikuwa imesema kwamba jaribio hilo lilihusisha injini yenye radio – isotope na lilifanyika katika ufukwe wa bahari.

Awali wizara hiyo ya ulinzi pia ilikuwa imesema kwamba mlipuko huo wa tarehe 8 Agosti ulihusisha injini ya roketi inayoendeshwa na maji na kutoa idadi ya waliofariki kuwa wawili bila ya kuelezea.

Kabla ya kichwa hicho , wizara ya ulinzi ililitangaza eneo La Dvina Bay kuwa eneo ambalo watu hawahitajiki kuwepo na kwamba litasalia kufungwa hao hadi mapema Septemba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles