22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Koeman atimuliwa Barcelona

CATYALUNYA, Hispania

HATIMAYE klabu ya Barcelona imemfuta kazi kocha wake raia wa Uholanzi, Ronald Koeman, uamuzi uliokuja baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Rayo Vallecano jana.

Koeman (58), aliajiriwa Agosti, mwaka jana, na msimu uliopita aliipa taji la Copa del Rey, ingawa alifeli kunyakua La Liga na ‘ndoo’ ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu huu pia umekuwa mbovu kwa upande wake, ambapo Barca imeambulia pointi tatu pekee katika mechi tatu za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, michuano ambayo iko chini ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).

“FC Barcelona imemuondosha Ronald Koeman katika nafasi yake ya kocha mkuu. Rais wa klabu, Joan Laporta, alimfahamisha juu ya uamuzi huu baada ya mechi ya Rayo Vallecano. Ronald Koeman ataaga Alhamisi (leo)…,” imesomeka taarifa ya klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles