25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WB yazuia misaada Sudan

KHARTOUM, Sudan

HATUA ya jeshi kupindua Serikali ya Sudan kimeendelea kuigharimu nchi hiyo na sasa Benki ya Dunia (WB) imesitisha misaada yake.

Baada ya mapinduzi hayo, maandamano makubwa yalijitokeza Jumatatu ya wiki hii nchini humo, huku kitendo hicho cha jeshi kikilaaniwa vikali na jumuhiya za kimataifa.

Adhabu waliyokuja nayo WB inatanguliwa na ile ya Umoja wa Afrika (AU) kutangaza kutoutambua uanachama wa Sudan kwa kuwa jeshi limechukua dola kinyume cha Katiba.

Huku pia Marekani ikisitisha msaada wa Dola za Marekani milioni 700, hiyo inaongeza presha kwa kiongozi wa mapinduzi hayo, Jenerali Abdel Fattah Burhan, katika kuharakisha mchakato wa kuunda Serikali ya kiraia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles