21.4 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha wa Katompa aomba radhi Watanzania

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

KOCHA wa bondia wa ngumi za kulipwa wa DR Congo, Erick Katompa, Lewis Mulamba, amewaomba radhi Watanzania kutokana na bondia wake kushindwa kufika nchini kuzichapa na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ baada ya kupata majeraha ya goti akiwa katika maandalizi ya mwisho.

Kocha wa Erick Katompa, Lewis Mulamba.

Katompa na Dulla Mbabe walitarajia kupanda ulingoni kesho Julai 15,2023 kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.

Kutokana na kushindwa kutokea kwa bondia huyo, Dulla Mbabe atapigana na Mkenya Denzel Onyango ambapo leo wamepima uzito tayari kwa pambano hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Lewis, amesema walikuwa tayari wamekamilisha maandalizi ya safari na walitarajia kukutana na Katompa uwanja wa ndege lakini hadi ndege inaondoka bondia huyo hakutokea kutokana na jeraha hilo.

“Tunaomba radhi kwa Watanzania kwa hili tukio la kukosekana Katompa, tulikuwa tayari kwa safari ya kuja Tanzania lakini mazoezi ya mwisho bondia akapata majeraha ya goti.

“Hakuna tatizo lingine, kuhusu suala la fedha nampongeza promota alikuwa amekamilisha Kila kitu. Nisema hii sio mwisho muda wowote Katompa atakapohitajika atakuja kucheza pambano na Dulla baada ya kupona,” amesema Mulamba.

Kwa upande wake promota wa pambano hilo, Meja Selemani Semunyu amesema kilichotokea ni changamoto ya tasnia hiyo ya masumbwi na kuwaomba radhi mashabiki wa mchezo huo, huku akiahidi burudani kesho kutokana na mabondia wengine wakali watakaopanda ulingoni.

Tofauti na pambano la Dullah Mbabe dhidi ya Onyango, mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni Nasibu Ramadhani dhidi ya Loren Japhet, Ramadhani Idd na Peter Toshi, Hassan Ndonga na Tasha Mjuaji, James Kibazange na Ramadhan Pido.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles