23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kidatu nayo kuzimwa

Tanesco-27April2015Na Mwandishi Wetu, Kidatu

SIKU moja baada ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kusimamisha uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Mtera, kituo cha kuzalisha umeme cha Kidatu kilichopo mkoani Morogoro  kinategemewa kuzimwa wakati wowote baada ya kupungua kwa kina cha maji.

Bwawa la Kidatu linazalisha megawati 204 lakini hivi sasa baada ya kina cha maji kupungua linazalisha megawati 27.

Taarifa ya kuzimwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kidatu ilitolewa jana na Meneja wa kituo hicho, Mhandisi Justus Mtolera, katika mkutano wake na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo.

“Bwawa la Kidatu tunazalisha megawati zaidi ya 200 lakini kwa sasa tunazalisha megawati 27 tu kwa kuwa bwawa la Mtera limekauka. Kujaa kwa bwawa la Mtera husababisha kujaa maji katika bwawa la Kidatu hivyo tunalazimika kusubiri mvua ienyeshe ndipo tuwashe.

“Hivi sasa tumelazimika kuwasha mashine moja kati ya nne. Kima cha juu cha ujazo wa bwawa hili ni lita za ujazo milioni 450 kutoka usawa wa bahari na ili mashine zote zenye uwezo wa kuzalisha megawati 50 zifanye kazi, zinahitaji kufikia ujazo huo lakini hadi kufikia jana kulikuwa na ujazo wa lita milioni 441.88,” alisema Mtolera.

Alisema kiwango cha maji kilichopo kina uwezo wa kuwasha mashine zote nne kwa siku nne tu, hivyo wamelazimika kuzima mashine tatu ili kubakisha moja inayozalisha megawati 27 na endapo maji yatapungua zaidi nayo itazimwa.

Mtorela alisema bwawa la Kidatu pia linapata maji kutoka mto Iyovu na Likosi ambayo pia yameanza kukauka na kuathiri uzalishaji umeme katika bwana hilo.

“Watanzania wanapaswa kuamini kuwa uhaba wa maji ndio unasababisha kuwepo kwa hali hii hivyo ni muhimu pia kwa watu wengine kufika katika eneo hili kujionea wenyewe hali halisi,” alisema Mhandisi Mtolera.

Juzi Tanesco ililazimika kusitisha uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Mtera baada ya mitambo yake kuzimwa kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika bwawa hilo linalozalisha megawati 80 ambacho ndicho kiwango cha juu kabisa kuzalishwa na bwawa moja hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles