29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli aunguruma nyumbani kwa Kikwete

g4Na Bakari Kimwanga, Bagamoyo

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kugundulika kwa gesi wilayani Bagamoyo kutatimiza ndoto yake ya kuijenga  Tanzania mpya ya viwanda.

Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo wilayani Bagamoyo, katika mikutano yake ya kampeni aliyoifanya kwenye majimbo ya Chalinze na Bagamoyo.

Alisema Tanzania mpya yenye kutoa ajira kwa vijana na kuwawezesha wanawake na wazee kiuchumi inakuja chini ya Serikali ya awamu ya tano, ambayo alitabiri yeye kuwa kiongozi wake.

“Kwanza niwapongeze wananchi wa Bagamoyo kwa kugundulika gesi hapa kwenu katika eneo la Ruvu. Na hii itasaidia sana kuijenga Tanzania mpya ya Magufuli ambayo itachochea ujenzi wa viwanda.

“Ukishakuwa na gesi, barabara za kutosha na umeme wa uhakika ni wazi vitasaidia sana ujenzi wa viwanda na kutoa ajira nyingi kwa vijana wa Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla,” alisema Dk. Magufuli.

Alisema kugundulika kwa gesi kutasaidia Mkoa wa Pwani na maeneo ya jirani kupaa kimaendeleo.

“Tanzania yetu Mungu anaipenda sana ndiyo maana na mimi nikaomba urais ili niweze kuijenga na hata kusimamia rasilimali za Watanzania kwa uadilifu, kikubwa ninawaomba mniamini na kunichagua kwa kura nyingi ili niwe rais wa Jamhuri ya Muungano,” alisema Dk. Magufuli.

Aidha Dk. Magufuli alimsifu Rais Jakaya Kikwete kuwa amefanya kazi kubwa ya kuiletea maendeleo Tanzania na hasa kuiinua kiuchumi.

“Rais wa awamu ya nne ametoka hapa Chalinze, Bagamoyo ameongoza kwa miaka 10, nami nimekuwa msaidizi wake kwa miaka 10. Alikuwa akinituma na kazi hii nimeifanya kwa umakini mkubwa, ikiwemo ujenzi wa barabara.

“Nami sasa nimeteuliwa na chama changu (CCM) kuwania nafasi hii, wana Bagamoyo na Watanzania kwa ujumla sitawaangusha, ninaomba mniamini ndugu zangu kwa kunichagua kwa kura nyingi,” alisema Dk. Magufuli.

Alisema anajua eneo la Chalinze watu wake hujishughulisha na kilimo, kikiwemo cha mananasi na kwamba serikali yake itahakikisha inajenga kiwanda cha kusindika matunda kama njia ya kupandisha thamani ya zao hilo kwa kuwa na soko la uhakika.

“Ninawaomba mnichagulie Ridhiwani awe mbunge wa Chalinze, ninahitaji kufanya naye kazi. Huyu ni mwanangu kabisa pamoja na kuwa ni mtoto wa rais, lakini hana majivuno.

“Na kwa upande wa Bagamoyo ninamhitaji Dk. Kawambwa (Shukuru), ni mchapa kazi mzuri jamani, ninawaomba mumchague kwa kura nyingi pamoja na madiwani wa CCM,” alisema Dk. Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles