30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

KANISA KATOLIKI LAGOMA KUMZIKA BILIONEA WA NGURDOTO

KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limekataa kuendesha misa ya maziko ya mfanyabiashara bilionea Faustine Mrema kwa madai hakuwa na Sakramenti ya ndoa na mke wake wala kipaimara.

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Theresia, Mtoto Yesu, Jimbo Kuu la Arusha Padri Festus Mangwangi amekiri suala hilo na kuongeza kuwa marehemu enzi za uhai wake hakuweka heshima na kanisa.

“Marehemu ni mkatoliki wa kuzaliwa, lakini hakuwahi kuwa na sakramenti ya ndoa na mke aliyezaa naye watoto wala kupata Kipaimara. Kanisa haliwezi kumzika kabisa, kawaida mazishi ya Kanisa Katoliki ni heshima inayotolewa kwa mhusika kama anastahili.

 

“Huyu hakuwahi kufunga ndoa kanisani, alijitenga na kanisa kwa hiyo kusema tumemtenga si kweli, yeye ndiyo alijikataa hakutaka kutafuta heshima yake na kanisa akiwa hai,” alisema Padri Mangwangi.

Kuhusu kutokwenda kwenye Misa za Jumuiya ambayo nayo ni moja ya taratibu muhimu inayowataka waumini wa kikatoliki kushiriki ibada za nyumba kwa nyumba Padri Mangwangi amesema, hata ibada hizo nazo pia marehemu alikuwa hashiriki.

“Jumuiya ni utaratibu wa kanisa unaowataka waumini wawe na ushirika wa karibu ikiwamo kufahamiana marehemu pia alikuwa hashiriki kabisa sasa unaanzaje kumzika mtu kwa heshima za Kanisa Katoliki?” amehoji Padri Mangwangi.

Wakati Kanisa hilo likijivua kushiriki Misa ya heshima ya maziko ya marehemu Mrema hiyo jana, Askofu Dk. Eliud Issangya wa Kanisa la Kimataifa la Kiinjili, alilazimika kuongoza Ibada hiyo ya maziko iliyofanyika Hoteli ya Ngurdoto, wilayani Arumeru.

 

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Kanisa AU MSIKITI huondoa ukatili KWA wanadam WENYE IMANI dhaifu huongezewa IMANI ZAO KWA kutendewa MEMA.wakati WOTE NA BILA YA KUJALI hali ya UCHUMI aliyonayo.IMANI dhaifu NI tofauti na mtu asuyeamini ALLAH (MUNGU) HIVYO kanisa AU MISIKITI isilipe Visasi KWA WATU WENYE Oman dhaifu. Wasilla Visasi kwa watu wenye iman dhaifu MISIKITI NA MAKANISA yanajiondolea HADHI yake KATIKA JAMII.
    WAISLAMU HUSEMA KWEBDA PEPONI NI MATENDO YA MTU MWENYEWE HAPA DUNIANI HUMFIKISHA PEOONI .SALA WAKATI WA MAZISHI ILE NI IBADA INAYOFANYWA NA WAKIOHAI WAKITARAJIA MAKIPO KUTOKA KWA ALLAH.NA MAREHEMU HAPOKEI THAWABU YA MTU ALIYEFABYA IBADA SIKU YA MAZISHI YAKE.NAFIKIRI HATA UKRISTO MANTIKI YA IBADA YA MAZISHI NI WALE WALIOHAI WAKIABUDU MUNGU NA KUTARAJIA MALIPO KUTOKA MUNGU KWA AJILI YA KUINGIA KWENYE UFALME MUNGU (KWA AJILI YA KWENDA MBINGUNI ) WANAOABUDU NA SI MAREHEMU.KWANI MAREHEMU HAWEZI KWENDA PEPONI KWA IBADA TU YA MTU MWINGINE HIVYO KANISA AU MSIKITI VISILIPE VISASI.UMUHIMU WAO KATIKA KUFARIJI KUWATIA MOYO WAKIOFIKWA NA MITIHANI NI MKUBWA SANA.MISIKITI NA MAKANISA VIWE NI VICHOCHEO VYA IMAN NDANI KAYA ZOTE KUWEPO KWAO NI MWANZO WA KUMUONDOA MWENYE SHIDA KATIKA DHIKI NA KUMUELEKEZA KWENYE PEPO KWA MWENENDO WA OMAN ALIYONAYO.UVUMILIVU UNATAKIWA
    KUONDOA MAMBO MABAYA NDANI KAYA ZETU NA HATIMAYE NCHI YETU.KUFUATA KITABU CHA MUNGU (VITABU VITAKATIFU KUR AN NA INJILI ) KUWAITA KWENYE NJIA YAKE ALLAH (MUNGU) NI JUKUMU ZITO NA NI MWITO. HAKUNA AWEZAYE KUFANYA KAZI YA MUBGU YA NGUVU NA REHEMA ZAKE ALLAH (MUNGU )VUTABU VYA MUNGU (VITABU VITAKATIFU) HAVILIPI VISASI KWA WENYE OMAN DHAIFU BALI HUWAITA KWA WAKATI WOTE NA WAKIWA KATIKA HALI YEYOTE
    VIONGOZI WA KABISA NA MISKITI WASILIPE VISASI WANADAMU NI DHAIFU SANA MBELE YA ALLAH (MUNGU).

  2. Hatuna budi kuwa waelekevu kwa mambo ya Mungu tunapokuwa hapa duniani. Kwani inatugharimu nini tunapokuwa wanyenyekevu mbele za Muumba? Kumbukeni leo na kesho na kwamba sisi ni wapita njia hapa ulimwenguni!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles