25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kaliua yatumia bil 9.9/- miradi ya maendeleo

Na ALLAN VICENT

-TABORA

JUMLA ya shilingi bil 9.955 zilizoidhinishwa na Serikali katika mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, zimetumika katika miradi ya maendeleo.

Kiasi hicho ambacho ni sawa na asilimia 49 ya bajeti yake yote, kilipitishwa na Baraza la Madiwani ili kitumike kukamilisha miradi mipya na viporo.

Akizungumza na MTANZANIA, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Dk. John Pima, alisema

utekelezaji wa miradi hiyo umefanyika kwa umakini mkubwa ikiwemo kutumia mfumo wa fosi akaunti ili kuepusha matumizi yasiyo na tija na kuwezesha kukamilika kwa wakati.

Alifafanua kuwa hadi kufikia Machi 31, mwaka huu halmashauri hiyo ilipokea kiasi cha sh bilioni 4.9 kutoka Serikali Kuu ikiwa ni sehemu ya fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.

Dk. Pima alibainisha kuwa halmashauri imetumia kiasi cha sh bil

4.7 sawa na asilimia 47 ya bajeti hiyo kwa kutekeleza miradi iliyoainishwa na baraza katika bajeti hiyo huku shughuli nyingine zikitekelezwa kwa kutumia fedha

zilizovuka mwaka.

Aliongeza kuwa halmashauri hiyo ilipokea Sh mil 428.4 kama fedha za bajeti ya nyongeza kutoka Serikali Kuu na wahisani ambazo zimepelekwa katika shule za msingi na sekondari kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.

Alitaja miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na fedha hizo kuwa ni ujenzi wa wodi ya mama na mtoto na ukamilishaji wa jengo la wagonjwa wa nje (ODP) katika hospitali mpya ya wilaya.

Miradi mingine ni ujenzi wa eneo la kuchomea taka katika hospitali ya wilaya kwa kutumia bajeti  iliyovuka mwaka kiasi cha Sh mil 13.2 ambapo fedha nyingine iliyotumika ni Sh mil 6 ikiwemo ufyatuaji wa matofali 5,000.

Alitaja miradi mingine kuwa ni ukamilishaji wa chumba cha upasuaji cha Kituo cha Afya Kaliua na ukarabati wa nyumba za watumishi ambapo kila mradi ulitumia bajeti iliyovuka mwaka ya Sh mil 12 na miradi hiyo sasa yote imekamilika.

Miradi mingine ni ukamilishaji wa jengo la ofisi, ujenzi wa uzio katika ofisi ya mkurugenzi, ukumbi wa halmashauri, vyumba vya walinzi na ujenzi wa stoo ambayo yote ipo katika hatua za mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles