28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Juninho kuachia ngazi Lyon

PARIS, Ufaransa

MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Lyon, Juninho, ametangaza kuwa ataachia ngazi ifikapo Januari, mwakani.

Kama itakumbukwa, Mbrazil huyo aliyewahi kuichezea kwa mafanikio timu hiyo, ameshikilia wadhifa huo kwa miaka miwili na nusu.

Kwa upande wake, uongozi wa klabu hiyo haujazungumza chochote juu ya taarifa hiyo ya Juninho kusema atajiuzulu.

Ikiwa atandoka, ni wazi Lyon italazimika kuingia sokoni kumtafuta mtu wa kushika nafasi hiyo kwa kuwa ni muhimu kwenye uendeshaji wa soka la kisasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles