WELLINGTON, New Zealand
NEW Zealand itapiga marufuku uuzaji wa tumbaku, lengo likiwa ni kukiondoshea kizazi kijacho utamaduni wa kuvuta sigara.
Katika sheria inayotarajiwa kuanza kufanya kazi mwakani, mtu aliyezaliwa baada ya mwaka 2008 hataruhusiwa kununua sigara au tumbaku kwa kipindi chote cha maisha yake.
“Tunataka kuhakikisha vijana hawaanzi kuvuta sigara,” amesema Waziri wa Afya, Dk. Ayesha Verall.
Wakati huo huo, madaktari na wataalamu wengine wa afya wameipongeza hatua hiyo. “Itasaidia watu kuacha (kuvuta) au kuhamia kwenye vilevi vingine visivyo hatari zaidi…” amesema Prof. Janet Hook, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Otago.