BEIJING, China
SERIKALI ya China imezionya nchi zilizogoma kushiriki michuano ya Olimpiki ya mwakani itakayofanyika Beijing, ikisema zitajutia hatua yao hiyo.
Marekani, Uingereza, Australia na Canada hazitapeleka wanamichezo wake, huku sababu ikiwa ni janga la Corona na kufikisha ujumbe wa kulaani vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu nchini China.
Ikizungumzia hulo, China kupitia kwa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, imesema: “Marekani, Uingereza na Australia zimetumia Olimpiki kama jukwaa la siasa.”
Kwa upande wake, Ufaransa ambao ni wenyeji wa Olimpiki ijayo, wameweka wazi kuwa hawataungana na mataifa yatakayogomea mashindano hayo ya Beijing yanayotarajiwa kufanyika Februari.