25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ATEMA NYONGO

Na Andrew Msechu, DAR ES SALAAM


Aweka wazi sababu za kumng’oa Mwigulu, amtaka mbunge aondoke CCM

RAIS Dk. John Magufuli, ametoa onyo kali kwa wabunge wa mikoa ya Kusini, wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao walikuwa wakipinga mipango ya Serikali kwa kivuli cha kutetea wakulima.

Amesema Serikali ipo tayari kuwapoteza wabunge hao.

Pamoja na hayo, kiongozi huyo wa nchi ameweka wazi kuchukizwa na matukio mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, likiwamo suala la mkataba wa Kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, huku akihoji watendaji waliopewa dhamana kuwa kimya na kushindwa kuchukua hatua, licha ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutoa maelekezo kwa Serikali.

Kauli hiyo aliitoa jana Ikulu Dar es Salaam wakati wa kuwaapisha mawaziri, manaibu waziri wapya na makatibu wakuu wa wizara, aliowateua juzi baada ya kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri.

Rais Magufuli alisema alikuwa akifuatilia Bunge la Bajeti lililomaliza vikao vyake juzi, huku akiweka wazi kutofurahishwa na baadhi ya wabunge waliokuwa wakitishia kuandamana kutokana na kufutwa kwa Mfuko wa Korosho.

Alisema wakati mijadala hiyo ikiendelea, alimpigia simu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, saa nane usiku na alimuuliza Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally kuhusu idadi ya wabunge wanaotoka mikoa ya Kusini.

“Nilimpigia simu Katibu Mkuu kumuuliza idadi ya wabunge wa mikoa ya Kusini akaniambia wapo 17, nikamwambia tunaweza kuwakosa wote na bado ‘coram’ (akidi) yetu bungeni ingetosha kuongoza Serikali.

“Na nilimwambia aanze mpango huo, ambapo hata Waziri Mkuu angeweza kuondoka kwa kuwa na yeye ni wa huko huko.

“Kuna mbunge mwingine alikuwa anataka umaarufu, eti anasema atachomewa nyumba. Walisema watafanya fujo, wafanye waone, nilimwambia Waziri Mkuu kama kuna shangazi zake ningeanza kupiga hao,” alisema Magufuli.

AMMWAGIA SIFA NAIBU WAZIRI

Akionyesha kufurahishwa na michango ya Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba, alisema hakumteua kwenye nafasi hiyo kama zawadi ila alivutiwa na michango yake ndani ya Bunge.

“Nimekuteua kwa sababu unastahili, nilikuona unapambana bungeni na kutetea ilani ya CCM wakati wa mjadala wa korosho,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles