20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

MKUU WA WILAYA ACHEKELEA UKARABATI WA CHUO KUENDANA NA THAMANI YA FEDHA

Hadija Omary, Lindi

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, Rukia Muwango, amesema ameridhishwa na ukarabati unaofanyika katika Chuo cha Ualimu Nachingwea kutokana na kasi ya ujenzi na thamani ya fedha zilizotumika.

Muwango ameyasema hayo juzi alipofanya ziara chuoni hapo ambapo pamoja na mambo mengine alikagua ukarabati wa majengo unaoendelea chuoni hapo.

“Sh milioni 900 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya shughuli za ukarabati unaosimamiwa na Mhandisi Mshauri wa Serikali, ukarabati huu ni wa kwanza kufanyika tangu chuo hiki kijengwe mwaka 1976,” amesema.

Hata hivyo, Muwango pia amemuagiza Mkuu wa Chuo kushirikiana na wanafunzi kulinda na kutunza  miundombinu hiyo baada ya ukarabati huo kukamilika ili iweze kutumika kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho,  Louis Letta amesema ukarabati unaofanyika chuoni hapo kwa sasa unahusisha majengo manane ambayo ni mabweni manne, jengo la utawala, maabara mbili, madarasa ya ghorafa tatu na vyoo vya nje na kwamba ukarabati huo unatarajia kukamilika juni 26, mwaka huu.

- Advertisement -
Previous articleSIRI NZITO BARUA KWA KKKT
Next articleJPM ATEMA NYONGO

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles