25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ANUNUA NDEGE MPYA SITA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli.

Na Bakari Kimwanga-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli, amesema kuwa hali ya uchumi wa nchi kwa sasa ipo vizuri na tayari ameshanunua ndege sita kwa ajili ya kufufua Shirika la Ndege la ATCL.

Hayo alisema jana Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua kikao cha NEC, ambapo alisema kwa sasa katika robo ya pili ya mwaka uchumi umepanda na kufikia asilimia7.2 huku matarajio kufikia mwishoni mwa robo ya mwisho ipande hadi asilimia 7.9.

Pamoja na hali hiyo amesema hali ya mfumuko wa bei imezidi kushuka na bado Serikali inaendelea kuchukua hatua zaidi ili kuweza kutimiza hatua ya kuwa na uchumiwa viwanda.

Kutokana na mkakati huo alisema kwa sasa Serikali imepanga asilimia 40 ya fedha zote zitakwenda kwenye miradi ya maendeleo.
“Licha ya hili pia tumepanga kwa mwaka huu wa fedha tutanunua meli mbili moja itakuwa Ziwa Victoria na nyingine Tanganyika.

“… sasa tumeshanunua ndege sita mpya kwa ajili ya kufufua shirika letu la ndege. Kati ya hizo tayari mbili zinaendelea kufanya kazi. Huwezi kujenga uchumi wa utalii kwa kutegemea ndege za jirani sasa tunajitaji kufikia watalii milioni mbili,” alisema Rais Dk. Magufuli

Alisema hadi kufikia Juni, 2017 ndege mpya mbili aina ya CS 3100 zenye uwezo wa kubeba abiria 137 hadi 150 huku ndege ya kubwa ya mwisho aina ya Dream Line ikitarajiwa kuwasili nchini Juni, 2018.

“Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 262 na ina uwezo wa kupaa kutoka Marekani hadi hapa bila kusimama popote. Na hili viwanja vingi vya ndege tutaweka lami ingawa sasa tumeanza na Dodoma.

“Tunapeleka haraka kwani shabaha yetu ni kuhakikisha tunajibu hoja 2020 wa namna tulivyotekeleza ilani ya uchaguzi,” alisema
Pamoja na hali hiyo alisema kuwa Sh bilioni 534 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini (REA) ambapo hadi sasa tayari wafadhili wameahidi kutoa Sh bilioni 200 ili kuunga mkono miradi hiyo.

“Si hivyo tu hata bajeti ya afya imepanda zaidi kwa Shilingi trilioni 1.99 ili kuwezesha ununuaji wa dawa. Si hilo tu pia tumeendelea na utekelezaji wa elimu bure kwa kutenga Shilingi bilioni18.77 kila mwaka,” alisema mkuu huyo wan chi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles