24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Joketi, Yamoto kumsindikiza Temba

jokatemwegeloi6NA THERESIA GASPER

MSANII wa kizazi kipya nchini, Aman Temba ‘Mheshimiwa Temba’, amesema wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Fundi’ ambao ameuachia rasmi jana utasaidia kuwafunda wanawake wanaoishi ndani ya ndoa.

Temba alisema imani yake ni kwamba, mashabiki wake watapokea vizuri wimbo huo kutokana na ujumbe mzuri uliopo ndani ya wimbo huo.

“Wimbo huu umetayarishwa na Marco Chali, katika studio ya Mj Record, ambapo nimeshirikiana na Joketi pamoja na Yamoto Band, pia kuna mwanadada anaitwa Asma ambaye naye sauti yake imetumika kunogesha wimbo huu,” alifafanua Temba.

Alisema pamoja na kuanza na wimbo huo anatarajia kuwapa mambo mazuri mashabiki wake ndani ya mwaka huu, huku akiwaomba wakae mkao wa kula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles