Umenitoa mbali ya Martha hadharani

0
868

injiliiNA MWANDISHI WETU

MWIMBAJI nguli wa nyimbo za injili Afrika Mashariki, Martha Nelson, amekamilisha wimbo wake mpya wa ‘Umenitoa Mbali’ alioundaa kwa muda wa miaka mitano.

Martha alisema kazi hiyo ina jumla ya nyimbo nane zenye ujumbe tofauti.

“Kazi hii niliiandaa kwa miaka mitano kwa lengo la kuifanya kuwa bora, hivyo niliifanya kwa utaratibu na uwezo wangu wote ndiyo maana leo hii imekamilika na ninatarajia kuweka sokoni wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Martha.

Katika hatua nyingine, Martha aliongeza kuwa albamu yake hiyo inatarajiwa kuzinduliwa katikati ya mwaka huu baada ya maandalizi yote kukamilika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here