24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 23, 2023

Contact us: [email protected]

Amshapopo: Mastaa walikataa kunisaidia kimuziki

amshapopoNA GLORY MLAY

MSANII wa kike anayekuja kwa kasi katika muziki wa kizazi kipya, Aisha Omary ‘Amshapopo’, amesema kwamba alikimbilia kwa msanii Barnaba Elias kwa kuwa wasanii wengine wenye majina walikataa kumsaidia kimuziki.

Asha alisema baada ya kuhangaika sana kurekodi studio zenye viwango vya chini alilazimika kwenda kwa wasanii wenye majina makubwa katika muziki huo kwa ajili ya ushauri na msaada lakini walikuwa wakimkwepa na kukataa kumsikiliza hadi alipokwenda kwa Barnaba.

“Nimeamini wasanii wa kike tuna wakati mgumu, nimehangaika kwa wasanii wakubwa lakini niliowafuata kwa msaada walikataa kunisaidia lakini nilipokwenda kwa Barnaba alinipokea akanikutanisha na prodyuza wake na akaniahidi kushirikiana naye katika nyimbo zangu mbili mpya ambazo nitarekodi katika studio yake,” alieleza kwa furaha msanii huyo.

Amshapopo alishawahi kurekodi nyimbo mbili ukiwemo ‘Amshapopo’ na ‘Amechoka’ ambazo hazikufanya vizuri kutokana na kurekodia katika studio zenye kiwango cha chini kwa ubora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles