32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la polisi Pwani laanika ripoti ya mwaka 2020

Na Gustafu Haule, Pwani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limeripoti kutokea kwa makosa ya jinai 1,791 mpaka kufikia Desemba 2020 ikilinganishwa na makosa 2,189 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Ripoti hiyo imetolewa leo Desemba 29, na Kamanda wa polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa alipokuwa akizungumza kuhusu mwenendo mzima wa makosa hayo kwa miaka miwili mfululizo.

Nyigesa amesema makosa ya jinai ya mwaka 2019 yalikuwa mengi na kwamba mwaka 2020 yamepungua kwa tofauti ya makosa 398 sawa na asilimia 18.2.

“Kupungua kwa makosa haya kumetokana na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kudhibiti makosa ya kibinadamu.

“Makosa hayo ni pamoja na mauaji, kubaka, wizi wa watoto, usafirishaji haramu wa binadamu, unyanga’nyi wa kutumia silaha, wizi wa mifugo, wizi wa magari, wizi wa uvunjaji, wizi wa pikipiki na uhalifu mwingine,” amesema Nyigesa.

Kuhusu ajali za barabarani, Nyigesa amesema waliweka mkakati ya kukabiliana na matukio hayo na kwamba mwaka 2020 wamefanikwa kupunguza ajali hizo kwa kiwango kikubwa.

Amesema, mikakati ya 2021 ni kuhakikisha mkoa unapunguza matukio ya uhalifu wa matukio ya ajali barabarani kwa kuimarisha doria katika maeneo yote na ukaguzi wa mara kwa mara.

Pia amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo hasa kupitia askari kata waliopo katika maeneo yao pamoja na vyombo vingine vya usalama ili kuufanya mkoa kuwa eneo salama la uwekezaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles