26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Askari Zimamoto aokoa mtoto mwingine chooni

ASKARI wa Jeshi la Zimamoto mkoani Kagera, Koplo Denis Minja kwa mara nyingine amefanikiwa kuwaongoza askari wenzake kumuokoa mtoto wa kiume wa miaka 2 akiwa hai aliyedumbukia chooni wakati akimfuata mama yake, Albina Paschael aliyekuwa bafuni.

Minja ambaye Mei mwaka huu alimuokoa mtoto mwingine wa kike wa mwaka mmoja aliyetupwa kwenye tundu la choo cha shule na kusababisha Kamishina Jenerali wa Jeshi hilo, John Masunga kumpandisha cheo na kuwa Koplo baada ya kufanya kazi nzuri aliyoifanya katika tukio hilo.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Kagera, Ispekta Hamis Dawa amesema katika tukio hilo lililotokea Desemba 28 mwaka huu saa 10 jioni maeneo ya Kayanga wilayani Karagwe, Minja alishirikiana na askari Norbert Saka, Eliad Batanyangwa na James Lukas kumuokoa mtoto huyo akiwa hai.

“Minja ambaye kituo chake cha kazi ni wilayani Ngara, kwa sasa anakaimu ukuu wa kituo cha Zimamoto na uokoaji cha wilayani Karagwe baada ya mkuu wa kituo hicho kwenda likizo lakini pia wilayani humo kwa ajili ya kumuuguza mke wake anayeishi wilayani humo.”

Kufuatia tukio hilo Dawa aliwashauri wazazi kuacha utamaduni wa kuongozana na watoto katika maeneo hatarishi kwani wana utamaduni wa kukariri maeneo wanayoendaga na wazazi wao na siku wakimtafuta wazazi wakawakosa wanaamua wanaenda kuwatafuta katika maeneo hayo hali inayosababisha wakumbane na matatizo kutokana na maeneo hayo kuwa hatarishi kwao.

Dawa alisema kwa sasa mtoto huyo aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Kayanga ameruhusiwa na anaendelea vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles