26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Jela miaka mitano kwa kusambaza Corona

MWANAUME raia wa Vietnam amehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kubainika kusambaza kwa makusudi virusi vya Corona.

Mahakama ilimkuta na hatia bwana Le Van Tri ilipojiridhisha kuwa aliwaambukiza Corona watu nane na mmoja kati yao alipoteza maisha.

Awali, Vietnam ilionekana kuidhibiti vilivyo Corona lakini kasi ya maambukizi ilizidi kuanzia Juni na hadi sasa waathirika ni 530,000 huku zaidi ya 13,300 wakipoteza maisha.

Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa na Mahakama, sehemu ya watu ambao Tri aliwaambukiza ni ndugu zake na adhabu ya kifungo itakwenda sambamba na faini ya Dola za Marekani 880 (zaidi ya Sh mil. 2 za Tanzania).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles