28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Watembezwa utupu kuita mvua

WAKAZI wa eneo linalokabiliwa na janga la ukame nchini India wametumia njia ya kuwatembeza utupu watoto wa kike kwa kile wanachoamini kitasaidia mvua kunyesha.

Katika tukio hilo lililotokea mjini Bundelkhand, watoto wa kike sita wenye umri mdogo wanaonekana wakiwa bila mavazi mbele ya umati, huku wakizunguka wakiwa wameshika fimbo zilizowekwa wadudu aina ya vyura.

Kwa mujibu wa imani za wakazi wa eneo hilo lililoko kwenye Jimbo la Madhya Pradesh, kitendo hicho kitamfurahisha mungu wa mvua na kuwaondolea balaa la ukame linalowatesa.

Aidha, Tume ya Kulinda Haki za Watoto ya India imelaani vikali, ingawa polisi wa eneo hilo wamesema hawajapokea taarifa rasmi juu ya kutokea kwa tukio hilo lakini wameanza uchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles