22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Huyu ndiye Black Coffee

Black Coffee.
Black Coffee.

LOS ANGELES, MAREKANI

NI nyota wa muziki nchini Afrika Kusini, jina lake halisi ni Nathi Maphumulo ‘Black Coffee’, ni mwimbaji, prodyuza na DJ mwenye kipaji kikubwa.

Amefanikiwa kutwaa tuzo ya Black Entertainment Television (BET) mwaka huu katika kipengele cha msanii bora wa kimataifa kutoka Afrika ‘Best International Act – Africa, huku akishindana na wasanii wenye majina makubwa Afrika akiwemo Nasibu Abdul (Diamond), Wizkid, A.K.A, Yemi Alade, Cassper Nyovest na Kiernan Forbes.

Black alizaliwa Machi 11, 1976, Nkosinathi mjini Durban na kukulia Eastern Cape nchini Afrika Kusini ni baba wa watoto wawili na mke wake ni Mbali Mlotshwa, walifunga ndoa mwaka 2011.

Black anamiliki studio inayoitwa Soulistic Music, mafanikio yake yalianza tangu mwaka 2003 kutokana na kutengeneza muziki wa Jazz na kuchaguliwa kuwa DJ bora katika tuzo za Red Bull Music Academy.

Licha ya kuwa na ulemavu wa mkono wa kushoto ambao mara kwa mara amekuwa akiuficha kwa kuuweka katika mfuko wa suruali yake hadi sasa ana jumla ya albamu tano.

Ulemavu wa Black ulitokana na ajali ya gari iliyoanguka kwenye kundi la watu zaidi ya 36 akiwemo msanii huyo na kusababisha kukatika kiganja chake cha mkono wa kushoto na mtu mwingine mmoja alipoteza maisha.

Mapema mwaka huu alipata mwaliko nchini Marekani katika onyesho la muziki lililoandaliwa na mkali wa rap, P. Diddy kwa ajili ya kuwa DJ wa onyesho hilo. Huyo ndiye Black Coffee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles