28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

50 Cent akamatwa kwa kutukana jukwaani

50 Cent
50 Cent

SAINT KITTS, CARIBBEAN

RAPA 50 Cent, juzi alijikuta katika wakati mgumu baada ya kukamatwa na polisi katika visiwa vya Caribbean kwa kosa la kutukana jukwaani.

Msanii huyo alikuwa anafanya shoo, hivyo alijikuta akitukana matusi baada ya DJ wake kupiga wimbo ulioshindwa kusikika kwa mashabiki 40,000 waliojitokeza kwenye shoo hiyo.

Kutokana na hali hiyo, 50 Cent alijikuta akitukana matusi na kuwafanya polisi wamsubiri amalize shoo hiyo kisha wamkamate na kumfikisha kituoni.

Baada ya kumalizana na polisi 50 Cent, aliwaomba radhi mashabiki wake kutokana na kauli yake ya kuonekana kuwa chafu.

“Najua shoo ilikuwa na mvuto wa hali ya juu, hivyo kutokana na hali kuwa tofauti nilishindwa kuzuia hisia yangu kwa kuwa nilitaka mashabiki waendelee kupata kitu bora, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa,” aliandika 50 Cent kwenye akaunti yake ya Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles