29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

HUKUMU ZA KIFO ZILIZOTEKELEZWA ZIMEPUNGUA DUNIANI

Idadi ya hukumu za vifo zilizotekelezwa duniani katika mwaka 2018 zimepungua hadi kiwango cha chini kabisa katika muongo mmoja, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na shirika linalotetea haki za binadamu la Amnesty International.

Ripoti hiyo imesema kiasi nchi 20 zilitekeleza hukumu hiyo kwa watu 690 mwaka 2018, ikiwa chini kwa asilimia 31 kutoka kiasi ya watu 993 waliouwawa katika mwaka 2017.

Katibu Mkuu wa shirika la Amnesty International, Kumi Naidoo amesema kwamba upunguaji huo mkubwa katika kutekeleza hukumu ya kifo unathibitisha kwamba hata zile nchi ambazo zina uwezekano mkubwa wa kutekeleza hukumu hizo zinaanza kubadilika na kutambua kuwa hukumu ya kifo sio jibu.

Shirika hilo limeeleza kupungua kwa utekelezaji wa hukumu hiyo katika nchi kama Iraq, Iran, Pakistan na Somalia.

Hata hivyo shirika hilo limeonya kwamba taarifa hizo zinachafuliwa na ukweli kwamba idadi ya utekelezwaji wa hukumu hiyo inaongezeka katika nchi kama Singapore, Belarus, Sudan kusini, Japan na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles