26 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

HAWA WA DIAMOND KUREJEA NCHINI BAADA YA MATIBABU 

Elizabeth Joachim, Dar es salaam



Hali ya msanii wa Bongo Fleva, Said Hawa  maarufu Hawa wa Diamond  imezidi kuimarika akiwa nchini India anakopatiwa matibabu ya ugonjwa wa figo.

Hali hiyo inaleta matumaini baada ya kuugua ugonjwa huo kwa zaidi ya mwaka na nusu. Meneja wa msanii wa muziki, Nassib Abdul (Diamond Platnum), Hamisi Shabani maarufu Babutale ameandika katika ukurasa wake wa instagram leo Ijumaa Novemba 9 akimshukuru  Mungu kwa aliyoyatenda kwa Hawa mpaka afya yake imeimarika.

“Asante Mungu, asante Watanzania kwa dua zenu Hawa sasa yupo salama kabisa  ameshatoa nyuzi na yupo tayari kurudi nyumbani, haikuwa kazi rahisi kupitia alipopitia pia tunaomba muendelee kutuombea ili tuwe na nguvu tuweze kuendelea  kumsaidia mwenzetu, nikikumbuka alivyonililia mama yake Hawa mpaka nilitamani nisirudi Tanzania ila majukumu mengine yalinifanya nirudi Amka uende kusali Mungu yupo na Dua pia zipo maana kila nikikumbuka lile tumbo la Hawa na leo halipo tena maana yake Mungu alitaka kuonyesha nguvu yake nakumbuka aliniambia lile tumbo amekaa nalo mwaka mmoja na nusu ila kwa nguvu ya Mungu limeondoka kwa Mwezi mmoja” ameandika Babu Tale

Aidha Baada ya MtanzaniaDigital kugundua Hawa anaumwa walifika na kimuhoji Octoba 20 ndipo Watanzania walipogundua ugonjwa uliokuwa ukimsumbua Hawa ambaye kupitia MtanzaniaDigital aliomba msaada kwa serikali, rais Magufuli na wadau wengine wa muziki na.afya wamsaidie kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu na akapata msaada wa kupelekwa India na msanii Diamond Platinum.

Hawa anatarajia kurejea nchini hivi karibuni baada ya hali yake kuonekana kutengamaa.

Naye Msanii  Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Nafarijika kuona tabasamu, sasa nitafurai kusikia wazo zuri la biashara kutoka kwako nikuwezeshe”

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles