26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Hati 1,900 za ardhi zatolewa Kagera

Renatha Kipaka, Bukoba

Hati za Ardhi 1,900 za ardhi zimetolewa kwa Wananchi mkoani Kagera kwa kipindi cha kuanzia Juni 2019 hadi 2021.

Hayo yameelezwa juzi na Msajili wa Hati Msaidizi, Nicolaus Mbwambo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake.

Amesema Mkoa umekuwa na migogoro mingi ya ardhi ambayo inaanzia nyumbani hivyo watu wakielimishwa tatizo hilo litakwisha.

Amesema katika kusaidia wananchi Wizara ya Ardhi ilifanya uhamisho wa ofisi za Kanda Juni 2019 kwa lengo la kusogeza huduma na kupunguza gharama kwa wananchi ambazo walikuwa wakizumia kumufata huduma hiyo Mwanza.

“Tangu Juni 2019 siku ambayo ofisi za kanda zimehamia hapa kutoka mkoani Mwanza, kumekuwa na mwitikio wa wananchi wanaofika ofisini kutafuta hati au ushauri na kupata huduma zao,” amesema Mbwambo.

Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kuhamia kwa ofisi hizo mkoani hapa tayari zaidi ya hati 2,400 zimesajiliwa kutoka maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Aidha, amesema upatikanaji wa hati kwa haraka itasaidia watu kutambua, umiliki wa mipaka yao na kuepuka migogoro inayojrudia.

“Ofisi zetu kuwepo Kagera hata sisi tunapata wasaa wa kuwahudumia kwa ukaribu tofauti tulivyokuwa mbali,” amesema Mbwambo.

Mbwambo amesema wananchi mkoani Kagera walijitahidi kuwaepuka vishoka na badala yake wafike ofisini kwangu wahudumiwe kwa ukaribu ili waweze kumiliki ardhi yao kwani ndio uti wa mgongo.

Kwa upande wake, Medard Mulisa ambaye ni Mstaafu anaishi Muhutwe wilayani Muleba amesema kunafaida mbili mtu anapokuwa na hati inakuwa nguvu za kumiliki ardhi kisheria.

Amesema kuwa faida ya pili hati inaweza kutumika kama dhamana kupata mkopo Benki.

“Nitumie nafasi hii kusema tu kuwa bado Kuna changamoto katika jamii watu hawajajua faida ya kumiliki hati hivyo niombe mamlaka zinazo husika katika ardhi kutoa elimu ya kutosha ili kuondoa migogoro,” anasema Mulisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles