21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

TIGO yazindua kampeni ya ‘Wagiftishe Gift juu ya Gift’

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Kampuni ya Tigo Tanzania imezindua kampeni mpya ya kufunga mwaka inayofahamika kama “WAGIFTISHE GIFT JUU YA GIFT” yenye lengo na dhumuni la kufanya sikukuu za mwisho wa mwaka kuwa za kipekee wa wateja wke nchi nzima ambapo watapata nafasi ya kushinda simu janja hadi 12 kila siku ndani ya wiki sita.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamis Novemba 18, jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi Meneja Mawasiliano kutoka Tigo, Woinde Shisael amesema kampeni hiyo ni kwa ajili ya wateja wapya na wazamani wa mtandao wa Tigo ambapo mteja atakayenunua simu janja ya ITEL T20 Sh 89,000 kutoka katika maduka ya Tigo nchi nzima watapata intaneti ya BURE GB 72 kwa mwaka mzima.

Aidha, amesema wakati huohuo ataingia kwenye droo ya kushinda simu janja 12 kila siku na pikipiki moja kila wiki kwa kipindi cha wiki sita.

“Kampeni hii inalenga kuongeza watumiaji wa simu janja nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza teknologia ya habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka 45% mwaka 2021 hadi 80% kufikia mwaka 2025.

“Pia kama mtandao unaoongoza kwa ubunifu na utoaji wa huduma za Kidigitali nchini kampeni hii itawawezesha wateja wetu kujipatia simu janja mpya na za kisasa alikadharika kuwanunulia ndugu, jamaa na marafiki huku wakijipatia mtandao wenye kasi zaidi wa 4G,” amesema Shisael.

Ameongeza kuwa kwa kipindi chote cha sikukuu za mwisho wa mwaka wateja wa Tigo wamekua wakifurahia ofa kabambe za punguzo la bei za simu pamoja na GIFT kemkem kwa ajili yao na ndugu zao.

“Sasa mteja atakayenunua simu janja ya ITEL T20 kwa ajili yake au familia yake kutoka maduka ya Tigo nchi nzima, atajijengea nafasi ya kushinda moja ya simu janja 504 au moja kati ya pikipiki 6 zitakazotolewa katika KAMPENI hii kwa kipindi cha wiki sita,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles