31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kupeleka milioni 500 kuboresha Afya

Safina Sarwatt, Mwanga

Serikali imeahidi kupeleka fedha zaidi Sh milioni 500 Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ili kitatua changamoto ya huduma za afya ukanda wa tambarare.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu ameyasema hayo Jumatano Novemba 17, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa inayotekelezwa kwa fedha kutoka mfuko wa UVIKO-19.

Waziri Ummy amesema serikali italeta fedha Sh million 500 kwa ajili ya kujenga majengo matatu kwa kuanzia ikiwemo jengo la mama na mtoto, maabara na jengo upasuaji na jengo la huduma ya wagonjwa wa nje.

“Serikali ya Mama Samia Suluhu ni ni ya maneno machache na utekelezaji tu, hivyo nawaagiza fedha zitakapoletwa hakikisheni ujenzi wa hospitali ya wilaya unaanza mara moja ili wananchi wapate huduma bora za Afya.

“Nimeridhishwa na miradi yenu mmefanya vizuri endeleeni kusimamia miradi kwa kuzingatia ubora kulingana na fedha zinazotolewa na serikali ya Mama Samia Suluhu,” amesema Waziri Ummy.

Awali akizungumza mbunge wa jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo amesema kuwa ujenzi wa hospitali ya wilaya moja ya ahadi ya rais wakati kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 na kwamba tayari eneo lenye ukubwa wa ekari zaidi 54 zimekwisha tengwa.

Amesema kuwa eneo hilo litatumika kwa ujenzi mradi wa hospitali ya wilaya pamoja na mradi wa chuo cha uganga na uuguzi na kwamba mradi huo utafungua fursa mbalimbali za kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Abdhalah Mwaipaya amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama nzuri na kwamba halmashauri ya hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles