24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

HANSPOPPE: TUNATAFUTA MBADALA WA MKUDE

Na ADAM MKWEPU-DARES SALAAM


mkude1Klabu ya Simba ipo katika mchakato wa kutafuta mbadala wa Jonas Mkude, baada ya nahodha huyo kutoonesha nia ya kuongeza mkataba.

Inadaiwa kuwa Mkude ambaye mkataba wake unamalizika Mei mwakani, amegoma kuongeza mkataba akitaka dau la usajili liongezwe kutoka Sh milioni 60 ya mkataba unaoisha hadi Sh milioni 80.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Zacharia Hanspoppe, alisema Mkude alikataa kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba na kuwazimia simu viongozi kwa siku tatu, huku akiwataka wazungumze na wakala wake, Juma Ndambile.

Alisema wameanza mipango ya kutafuta mchezaji mwenye uwezo zaidi yake katika nafasi ya kiungo mkabaji.

“Kama mchezaji anaringa, ni vyema kutafuta mbadala wake ili anyooke, tunaamini angekuwapo Justice Majabvi, jambo hili lisingetokea na wala Mkude  asingesumbua,” alisema Hanspoppe.

Hanspoppe alisema Mkude anataka kupewa dau kubwa kama wanavyosajiliwa wachezaji wa kimataifa, lakini kiwango chake ni cha kawaida hivyo wanaona ni bora kufanya uamuzi mapema katika usajili wa dirisha dogo.

“Mkude ni mchezaji ambaye tumemkuza wenyewe na kumkabidhi majukumu ya unahodha, lakini anajifanya amekua na wakati hata asipokuwepo kwenye timu hatupati madhara yoyote,” alisema Hanspoppe.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Simba umemtaka mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, asitegemee kwamba klabu hiyo itamsajili katika dirisha dogo kutokana na maudhi aliyowapa mashabiki wa timu hiyo alipojiunga na Wanajangwani msimu wa 2014/15.

“Kwa sasa, Simba kumsajili Tambwe ni ndoto kwani alitusema ovyo sana wakati anakwenda Yanga, kitendo ambacho kiliwaudhi sana viongozi na mashabiki,” alisema Hanspoppe.

Straika huyo raia wa Burundi, aliueleza uongozi wa Yanga kuwa hawezi kuongeza mkataba mpya kama watashindwa kumshawishi kwa kumuongezea dau mkataba wake utakapomalizika Mei mwakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles