23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TAASISI YAIPA TBL TUZO BORA YA UAJIRI

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


pg-24TAASISI ya kimataifa ya masuala ya rasilimali watu na ajira ijulikanayo kama Top Employer Institute yenye makao yake makuu nchini Uholanzi, imeitunukia Tuzo ya Mwajiri Bora 2017 Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kutokana na kuzingatia na kutekeleza kanuni za rasilimali watu na uajiri ipasavyo.

TBL ilitangazwa rasmi kuwa mshindi wa tuzo hii katika hafla iliyofanyika Johanesburg nchini Afrika Kusini mapema Oktoba mwaka huu.

Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo ilifanyika katika Kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na menejimenti na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa taasisi ya Top Employer Institute Kanda ya Afrika, Billy Elliot, alisema suala kubwa ambalo limeangaliwa ni jinsi wafanyakazi wanavyopata fursa ya kujiendeleza binafsi na kukuza taaluma zao
“Baada ya kufanya tathmini ya vigezo vyote hivi, tumebaini TBL inakidhi kiwango cha kuwa mwajiri bora nchini Tanzania,” alisema Elliot.

Aliongeza kuwa vigezo vya ushindi vimetokana na utafiti wa taasisi ya Top Employers kwa makampuni mbalimbali makubwa nchini kwa lengo la kuona utekelezaji kanuni za ajira na rasilimali watu ambapo kampuni ya TBL imebainika kuwa na vigezo vya ubora katika utekelezaji wa kanuni za ajira kwa mwaka ujao 2017.

Baadhi ya vigezo vilivyofuatiliwa katika utafiti huo ni mikakati ya kukuza vipaji vya wafanyakazi, mpangilio wa kazi wa kila siku, mazingira ya kazi, uendelezaji wafanyakazi kimafunzo, utawala sehemu za kazi, taaluma, upandishaji vyeo, masilahi ya wafanyakazi, malipo ya stahiki zao kwa ujumla na desturi ya kampuni.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL, David Magese, alisema: “Hatua hii ya kampuni yetu kutangazwa kuwa Mwajiri Bora na taasisi ya kimataifa ya Top Employers Institute ni uthibitisho kuwa tumekuwa tukitekeleza kanuni bora za rasilimali watu na uajiri ambayo msingi wake mkubwa ni kujali masilahi ya wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles