30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MTEULE GAMBIA KUACHIA HURU WAFUNGWA

BANJUL, GAMBIA


adama-barrowIKIWA ni mara ya kwanza tangu ashinde uchaguzi wiki iliyopita, Rais Mteule wa Gambia, Adama Barrow ameeleza hatua atakazochukua, ikiwamo kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa.

Barrow, ambaye alikuwa akifanya kazi kama mfanyabiashara wa kujenga majumba na kuuza, alimshinda Rais Yahya Jammeh, aliyenyakua madaraka kwa mtutu wa bunduki miaka 22 iliyopita.

Makundi ya haki za binadamu yamemlaumu Jammeh kwa ukiukaji wa haki za binadamu ikiwamo dhidi ya wanahabari, wanasiasa za upinzani na watu wajihusishao katika mapenzi ya jinsia moja.

Barrow amewahimiza watu walioikimbia Gambia kwa sababu ya hali ngumu ya maisha wakati wa mtangulizi wake kurudi nyumbani ili kusaidia kujenga taifa lao.

Aidha alirudia msimamo wake kwamba atabadili mpango wa awali wa Jammeh wa kutaka kuiondoa Gambia kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), na Jumuiya ya Madola.

Hayo yanakuja baada ya Jammeh, kiongozi wa muda mrefu, kulishangaza taifa hili dogo la Afrika Magharibi kwa kukubali kushindwa katika uchaguzi huo.

Katika taarifa yake Jammeh alimpongeza Barrow na kumtakia kila la heri pamoja na Wagambia wote na kuongeza kuwa ulikuwa ni ushindi wa wazi.

Kauli yake hiyo iliyorushwa katika redio ya taifa ilichochea sherehe kubwa nchini kote, ambapo wengfi walikesha usiku kuchwa kusherehekea ushindi na ondoko la Jammeh.

Jammeh, amgbaye amesema kuwa ataendelea na shughuli zake za kilimo aliongoza kwa mkono wa chuma baada ya kushika madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi miaka 22 iliyopita.

Lakini kuna wasi wasi bado kuhusu namna atakavyoachia madaraka na iwapo jeshi tiifu kwake litakuwa tayari kubadilika na kumuunga mkono Barrow.

Barrow pia anakabiliwa na changamoto nyingi katika Taifa hili dogo na maskini, ambalo wananchi wengi vijana wametorokea mataifa ya ng’ambo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles