29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri Geita kupewa Sh bilioni 9.2 na GGM

 MWANDISHI WETU -GEITA

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) na Halmashauri ya Mji wa Geita, wamesaini makubaliano ya utekelezaji wa Mpango wa Kusaidia Jamii (CSR) kwa mwaka 2020 wenye thamani ya Sh bilioni 9.2. 

Makubaliano hayo yamethibitisha ahadi ya GGML kwa Serikali baada ya kutekeleza mabadiliko yaliyomo kwenye kifungu cha 105 cha Sheria ya Madini ambacho kinajumuisha utekelezaji wa CSR.

Utekelezaji wa CSR utanufaisha jamii ya Geita katika maeneo ya mazingira, miundombinu, afya, elimu, biashara ndogo na za kati.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel alisema Serikali inathamini ushirikiano uliopo kati ya GGML na jamii ya Geita.

Alisema GGML inajitahidi kusaidia Serikali kuwa na maendeleo endelevu ya jamii na uchumi katika jamii ya mji wa Geita. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson, alisema hatua hiyo inatekeleza malengo ya kampuni hiyo kuendeleza ushirikiano na Serikali za mitaa na jamii nzima kwa ujumla katika kutambua na kusimamia miradi muhimu kwa mustakabali endelevu wa Mkoa wa Geita.

“Tunafurahi sana kuendeleza ahadi yetu kwa Serikali na jamii wenyeji. Katika mwaka huu wa tatu wa utekelezaji wa mpango huu baada ya mabadiliko ya sheria ya madini, ni matumaini yetu kuwa tunaweza kuendeleza tulipoishia katika miradi iliyopita.

“Tangu GGML ianzishwe, imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mkoa wa Geita kusaidia miradi kadhaa ya kijamii kupitia ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi (PPP) sanjari na mipango ya kitaifa.

“Pamoja na tunu yake kuu ya kusaidia jamii ya Geita kuwa na maendeleo endelevu kijamii na kiuchumi ambayo yatabakia hata baada ya shughuli za uchimbaji kumalizika, pia kampuni imefadhili utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwamo usambazaji wa maji safi, uendelezaji wa shughuli za uchumi katika sekta za kiimo, ujenzi na huduma,” alisema Jordinson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles