26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Zungu ataka madai mbegu za GMO kuleta njaa yachunguzwe

RAMADHAN HASSAN -DODOMA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Musa Zungu, ameagiza  kuchunguzwa  kwa mbegu za uhandisi jeni (GMO) zinazodaiwa kuwa na viashiria vya kuendeleza njaa barani Afrika ili kujua kama kweli zinafaa kwa matumizi na zitaweza kusalia nchini na bara la Afrika kwa kipindi kirefu.

Agizo hilo alilitoa jana jijini hapa wakati alipokuwa akizindua Kamati ya Kitaifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa.

Alisema kuna ambazo hazijadhibitika zikidaiwa inawezekana kuna baadhi ya mbegu za GMO ambazo zimeletwa Afrika kwa mkakati mrefu wa kuendeleza njaa barani Afrika.

“Hii ni kazi yenu kuchunguza na kuthibitisha kama hizi  kweli zinafaa  na ni endelevu na zitaweza kusaidia Tanzania na Bara la Afrika kwa kipindi kirefu.

“Kuna vita kubwa duniani inayokuja sasa hivi, ni ya chakula na maji, kukosekana kwa vitu hivi taifa  litaangamia, lakini tunaamini majukumu na uzalendo mliopewa mtasimamia vizuri tafiti zenu na mtaishauri vizuri Serikali ili tujue ni njia ipi sahihi ambayo Tanzania itaitumia,” alisema Zungu.

Alisema anakumbuka mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka ya nyuma  haukutumika vizuri nchini, lakini ulitumika vizuri nje ya nchi miaka ya 80 na 90.

“Mpango wa maendeleo ya nchi yetu ulichukuliwa na nchi zingine, lakini sisi wenyewe tuliyaweka chini ya meza.

“Lakini kwa awamu hii ya tano mabadiliko mnayaona ya Rais John Magufuli, kwa uzalendo wake na upembuzi wake wa taifa lake taifa letu ‘lina-progress’ na litaendelea ‘ku-progress’ na tafiti na maoni na mapendekezo ambayo mtaipa Serikali ili tuweze kuvuka na taifa letu,” alisema Zungu.

Alisema katika kutekeleza matakwa ya itifaki hizo, Serikali iliandaa kanuni ya usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa za mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2015.

Aidha, kifungu cha 9 cha kanuni hizo kimempa mamlaka ya kuteua wajumbe wa kamati watakaohudumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

“Kwa muktadha huo, nimewateua kuwa wajumbe wa kamati hii. Hivyo nichukue fursa hii kuwapongeza wote kwa kuteuliwa kuchukua jukumu hili muhimu kwa taifa letu,” alisema Zungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles