22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

GUARDIOLA AWAOMBEA RADHI ARGUERO NA FERNANDINHO

MANCHESTER, ENGLAND


pep-guardioloa

KOCHA wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, amewaombea radhi wachezaji wake, Sergio Aguero na Fernando Roza, kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Etihad, kikosi cha Guardiola kilipokea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Chelsea, huku mashabiki wa uwanja huo wakishuhudia nyota wao wawili wakioneshwa kadi nyekundu.

Wachezaji hao walioneshwa kadi hizo katika dakika ya 90 kutokana na Arguero kucheza mchezo ambao si wa kiungwana kwa beki wa klabu ya Chelsea, David Luis.

Baada ya kumchezea vibaya, baadhi ya wachezaji wa Chelsea walionekana kumzonga Arguero na kuanza kurushiana maneno, hivyo Fernandinho naye alionekana kuja kumtetea Aguero na kusababisha kugombana na kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas.

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, inaonesha kuwa Fabregas alikuwa wa kwanza kumpiga kofi Fernandinho, hivyo na yeye alirudisha na kuamua kumsukuma hadi kuangukia nje ya uwanja, hivyo mwamuzi aliamua kumuonesha kadi nyekundu mchezaji huyo.

“Mchezo ulimalizika bila ya kuwa na amani, ni muwazi kwamba sijapenda kilichotokea uwanjani, hivyo ni bora nikaomba radhi kwa mashabiki pamoja na wadau wa soka kutokana na utovu wa nidhamu ambao umeoneshwa na wachezaji wangu.

“Sijui kama Aguero alikusudia kucheza vibaya, lakini hicho ndicho kilichotokea, wachezaji wote wawili wana uwezo mkubwa na sikutegemea kama watafanya hivyo, hata hivyo nimeshangaa kuona Fernandinho akienda kumtetea Aguero.

“Wakati Nolito alipofanya hivyo katika mchezo dhidi ya Bournemouth, ilikuwa ni kadi nyekundu na kusimamishwa michezo mitatu na ndio maana Fernandinho alikwenda kumtetea mchezaji mwenzake.

“Hadi sasa sijafanya mazungumzo yoyote na wachezaji hao kutokana na kile kilichotokea, lakini ninaamini tutaona katika TV kuona nini kilitokea,” alisema Guardiola

Hata hivyo, kocha huyo aliongeza kwa kusema kwamba, timu yake imepoteza mchezo huo kutokana na kukosa nafasi nyingi ambazo walizipata na si kwamba tatizo la mwamuzi, lakini Man City itakuwa na wakati mgumu wa kutwaa ubingwa kutokana na kutengeneza nafasi 14 na kupata bao moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles