31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WENGER: ALEXIS SANCHEZ NI HABARI NYINGINE

LONDON, ENGLAND


alexis-sanchezKOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amemmwagia sifa mshambuliaji wake, Alexis Sanchez, kutokana na kiwango alichokionesha kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki dhidi ya West Ham.

Katika mchezo huo, Arsenal ilifanikiwa kushinda mabao 5-1, huku mshambuliaji huyo akiweka historia yake kwa kufunga mabao matatu (hat trick) ndani ya dakika 14, hivyo kuzidi kumchanganya kocha huyo.

Katika mchezo huo ambao ulikusanya watazamaji 56980 huku West Ham wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani, walijikuta mashabiki wao wakitoka uwanjani mmoja mmoja baada ya kichapo hicho katika dakika za lala salama.

Wenger ameweka wazi katika ulimwengu huu wa soka kuwa washambuliaji bora wanaofanya vizuri duniani wanatoka America Kusini, hivyo kati ya washambuliaji hao ni pamoja na mchezaji wake Sanchez.

“Sanchez anazidi kuonesha ubora wake katika soka, katika ushindi wetu wa mabao matano, ametoa mchango mkubwa, hapa ni sehemu yake sahihi na ndio maana anaonesha kiwango cha hali ya juu.

“Ameweza kuweka historia mpya ya kutumia dakika 14 kufunga mabao matatu, huku ikiwa ni mara yake ya pili kupachika mabao matatu katika ligi tangu ajiunge na klabu hii.

“Mchango wake ni mkubwa ndani ya klabu, kama atacheza chini ya kiwango basi timu hiyo itakuwa katika wakati mgumu na kama akiamua kucheza katika kiwango chake, basi inakuwa kazi rahisi kwa wachezaji wengine kuonesha uwezo wao,” alisema Wenger.

Kocha huyo mbali na ushindi alioupata, lakini amekisifia kiwango ambacho West Ham walikionesha ndani ya dakika 90.

“Ni wazi tumecheza na timu bora sana katika ligi kuu, wameonesha kupambana kwa dakika 90, lakini kitu ambacho tutaendelea kujilaumu ni kwamba tumeshindwa kutumia nafasi nyingi katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, ninaamini kama tungeweza kufanya hivyo basi tungekuwa na mabao mengi zaidi.

“Lakini kwa kuwa wachezaji wangu walishindwa kufanya hivyo katika kipindi cha kwanza, basi waliweza kupambana kwa ajili ya kipindi cha pili na waliweza kutumia nafasi walizozipata,” aliongeza.

Kwa upande wa kocha wa klabu ya West Ham, Slaven Bilic, amedai kuwa amepoteza mchezo huo mbele ya timu bora na walishindwa kuzitumia nafasi walizozipata.

“Ninaamini tunaweza kufanya vizuri msimu huu kama ilivyo msimu uliopita, lakini hatuwezi kushinda katika kila mchezo, kuna wakati tunaweza kufanya vizuri na wakati mwingine tunapoteza, lakini bado tuna nafasi ya kuendelea kufanya vizuri.

“Kwa matokeo haya, naomba nitumie nafasi hii kuomba radhi kwa mashabiki wa klabu hii pamoja na wadau wa soka kutokana na matokeo mabaya tuliyoyapata, ni wazi kuwa ni mabaya.

“Tupo katika kipindi kigumu hasa katika kushuka daraja, lakini ninaamini wachezaji wote wanalijua hilo na wanapambana kuhakikisha tunabaki kwenye ligi,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles