26.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

GUARDIOLA ATANGAZA KUSTAAFU KUFUNDISHA SOKA

MANCHESTER, ENGLAND


pep-guardiola

KOCHA wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, amedai kuwa hana mpango wa kuendelea kufundisha soka hadi kufikia umri wa miaka 65 kabla ya kuachana na kazi hiyo.

Guardiola mwenye umri wa miaka 45, raia wa nchini Hispania, klabu yake ya kwanza kufundisha ilikuwa ni Barcelona, ambapo alianza majukumu yake tangu 2008 akitokea kufundisha timu B, kabla ya kuondoka mwaka 2012 na kujiunga na Bayern Munich ya nchini Ujerumani ambapo hapo aliondoka majira ya joto mwaka jana na kujiunga na Man City.

Kutokana na hali hiyo, hadi sasa kocha huyo amefundisha jumla ya klabu tatu kubwa barani Ulaya, lakini amedai kuwa lengo lake ni kufundisha soka hadi pale atakapofikisha miaka 60 au 65 na ndipo atatangaza kustaafu rasmi soka.

“Nitaendelea kuwa hapa Manchester City kwa misimu mitatu labda na zaidi, sina mpango wa kuendelea kufundisha soka kwa muda mrefu kama ilivyo kwa makocha wengine duniani, nafikiri mchakato wa kuanza kusema kwa heri unakaribia,” alisema Guardiola

Guardiola ameshinda vikombe 14 katika miaka minne akiwa na klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, ikiwa ni pamoja na vikombe vitatu vya ligi kuu na viwili vya ligi ya mabingwa Ulaya.

Kocha huyo baada ya kuachana na Barcelona, alipumzika mwaka mzima kabla ya kujiunga na Bayern Munich na kuwaongoza kupata vikombe vitatu vya ligi kuu licha ya kukosa ligi ya mabingwa Ulaya kama ilivyo kwa Barcelona.

Lakini hali imekuwa ngumu katika michuano ya ligi kuu nchini England kama ilivyo urahisi kwa ligi ya nchini Hispania na Ujerumani.

Kwa sasa kocha huyo na kikosi chake cha Man City wanashika nafasi ya tatu kabla ya michezo ya jana kuendelea nchini England, hivyo amekubali kuwa kuna ugumu mkubwa katika ligi hiyo tofauti na ligi nyingine alizopita kocha huyo.

Kocha huyo aliwahi kusema kwamba, hajawahi kufukuzwa kazi kutokana na matokeo mabaya, lakini kutokana na ushindani uliopo ndani ya nchi ya England kuna uwezekano mkubwa wa kufukuzwa kazi.

Katika mchezo wao wa juzi, timu huyo ilifanikiwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Burnley, ushindi huo waliupata japokuwa walikuwa pungufu baada ya kiungo wao Fernandinho kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu, ila mabao ya Gael Clichy na Sergio Aguero yaliwapa ushindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles