31.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Giggs aipa Liverpool ubingwa England

ryan-giggs-man-united_3131822LIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA msaidizi wa zamani wa timu ya Manchester United, Ryan Giggs, anaamini kuwa klabu ya Liverpool ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu na misimu mingine inayofuata.

Giggs amedai kuwa kocha mpya wa klabu hiyo, Jurgen Klopp, ana mipango ambayo itawafanya Liverpool kutwaa taji msimu huu japokuwa kuna ushindani mkubwa dhidi ya Man City, Man United na klabu nyingine.

Liverpool ikiweza kutwaa ubingwa huo mwaka huu itakuwa ni mara ya kwanza tangu ligi hiyo kuanzishwa mwaka 1992, lakini Gisggs anaamini klabu hiyo inaweza kushinda msimu huu na misimu mingine ijayo.

“Liverpool msimu huu inaweza kuwashangaza wengi kama ilivyo kwa Leicester City msimu uliopita, siwezi kuwazungumzia United kwa kuwa wamekuwa na historia kubwa katika kushinda taji hilo.

“Ninachokiamini ni kwamba hakuna klabu ambayo itaweza kuweka historia kama ambayo iliwekwa na United tangu miaka ya 90, kilichopo kwa sasa ni kupishana.

“Kila klabu inataka ushindi, lakini Liverpool inaonesha nia kwamba inataka ubingwa kwa mara ya kwanza, inaweza kufanya hivyo kutokana na uwezo wa kocha wao Klopp na kama watashindwa msimu huu basi wataweza kufanya hivyo msimu ujao,” alisema Giggs.

Hata hivyo, nyota huyo amedai kuwa Liverpool ilipata mafanikio makubwa ikiwa na nahodha wao, Steven Gerrard ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya LA Galaxy tangu msimu uliopita.

Mchezaji huyo akiwa na Liverpool aliweza kuipa klabu hiyo ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya pamoja na Kombe la FA, lakini alishindwa kuipa ligi kuu.

“Ninajaribu kuiangalia Liverpool kwa sasa tangu kuondoka kwa Steven Gerrard, bado sijaona nyota ambaye anaweza kuwa kiongozi wa timu kama mchezaji huyo. Wapo wachezaji ambao wanafanya vizuri kama vile Philippe Coutinho, Jordan Henderson, lakini bado hawajafikia uwezo wa Gerrard.

“Hii ni sawa sawa na klabu ya Man United baada ya kuondoka kwa nyota Roy Keane mwaka 2005, ilikuwa ni sawa na kuondoka kwa wachezaji wawili ndani ya klabu hiyo lakini baadaye klabu ilikuja kukaa sawa,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles