24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Conte: Nina wasi wasi na moyo wangu

conteLONDON, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, ameweka wazi kuwa ana wasi wasi na moyo wake katika kila mchezo ambapo klabu yake ya Chelsea ikishuka dimbani.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Juventus, amedai kuwa ligi kuu nchini England ina ushindani mkubwa, hivyo kila wakati anakuwa na wasi wasi wa kufanya vibaya huku timu yake ikishuka dimbani.

Chelsea ilipoteza michezo miwili mfululilo dhidi ya Arsenal na Liverpool, lakini baadaye ilionesha uhai na kuweza kufanya vizuri dhidi ya Manchester United kwa kushinda mabao 4-0 pamoja na kufungwa mabao 2-1 dhidi ya West Ham katika Kombe la Ligi, hivyo Conte amedai kuwa anaumizwa na matokeo hayo.

“Nina wasi wasi na moyo wangu, lakini katika msimu huu nitahakikisha ninafanya kila liwezekanalo ili niweze kufanya mazoezi binafsi kwa ajili ya kuweka sawa mambo yangu.

“Najua ni hatari lakini natakiwa kuweka mfumo wa GPS kwa ajili ya kuangalia moyo wangu kila wakati timu yangu ya Chelsea ikishuka dimbani,” alisema Conte.

Kocha huyo aliongeza kwa kusema kuwa kila akipata muda anaweza kufanya mazoezi ya kukimbia kwa dakika 30 hadi 40 kwa ajili ya kujiweka sawa.

“Nikimaliza kuwafundisha wachezaji wangu kama ninakuwa na muda nautumia vizuri kwa ajili ya mazoezi binafsi ili nijiweke sawa, tuna viwanja vinne hapa hivyo ninapata nafasi ya kujichanganya na viongozi wenzangu kwa ajili ya kufanya mazoezi.

“Wakati ninaanza kucheza soka nilikuwa nakula vizuri, lakini tangu nimekuwa kocha sina amani sana kwa kuwa muda wote ninakuwa ninaifikiria timu yangu.

“Lakini natarajia kurudisha hali yangu ya awali ili niweze kuwa na amani, kama nashindwa kufanya mazoezi chakula kinakaa mwilini bila mpango, lakini ukiwa unafanya mazoezi afya inakaa vizuri.

Chelsea leo hii inashuka dimbani dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa St. Mary, hivyo Conte anaamini kuwa ana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.

“Kesho (leo), tutakuwa ugenini dhidi ya wapinzani wetu Southampton, tunaamini tutafanya vizuri, lengo letu ni kushinda katika kila mchezo na sasa nguvu zetu tunazihamishia huku kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika Kombe la Ligi,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles